Asili Yetu © All rights reserved
Huyu ni CHURA aina ya NINJA aliyegunduliwa mwaka 2011 New York nchini Marekani, ikiwa ni baada ya kupimwa DNA na kugundulika kuwa Chura aina ya NINJA yuko tofauti na Vura wengine tuliowazoea japokuwa chura huyu alikuwepo bila kugundulika kabla.
"HORROR WASP"
Mdudu huyu amegunduliwa rasmi mwaka 2011 katika kisiwa cha SULAWESI huko INDONESHIA japokuwa mdudu huyu alikuwepo kabla. Mdudu huyu ameonekana kuwa wa ajabu kutokana na viungo vyake kuwa vikubwa tofauti na wadudu wengine.
"MICRO" CHAMELEON
Huenda ukawa na mashaka katika picha hii, kwasababu kinyonga huyu amesimama katika njiti ya kiberiti, lakini takwimu zinaonyesha kuwa "MICRO" ni kinyonga mdogo sana mwenye urefu wa inchi 0.63 bila mkia, hivyo kuweza kutoshereza kusimama katika njiti ya Kiberiti. Kinyonga huyu amegundulika katika kisiwa cha MADAGASCA mwaka huu wa 2012.
"JOKER" CRAB
"Kaa" huyu ambae jina lake la kisayansi anaitwa "Insulamon palawanese" aligundulika katika kisiwa cha "PALAWAN Ufilipino" mwaka 2012 ambako ndiko anakopatikantu katika dunia hii.
"MATILDA" VIPER
Nyoka huyu anayejulikana kwa jina la "MATILDA" ni miongoni mwa nyoka chache hatari zilizogundulika Afrika (yani Tanzania). Nyoka huyu anamapembe mawili kichwani mwake ambayo huweza kukua hadi urefu wa sentimita 65 huku zikiwa na sumu kali. Nyoka huyu aligundulika mwaka 2010 na wanasayansi na kumpatia jina la Matilda baada ya mtoto wa miaka saba (7) wa mwana Sayansi kumpatia jina hilo.
Mjusi huyu aligundulika mwaka 2011 katika kisiwa kidogo cha "HON KHOAI".
"STABBING" SHARK
Samaki huyu aligundulika nchini MOZAMBIQUE mwaka 2011.
"YODA" BAT
Popo huyu amegudulika mwaka 2009 katika msitu wa PAPUA huko GUINEA MPYA. Mnyama huyu bado hajapata jina maalum.
"YET" CRAB.
Mdudu huyu aligundulika mwaka 2005.
Hii ni mara yangu ya kwanza kumuona tumbili akiwa na aina hii ya pua!!!!!! Na wewe je?










No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA