Header Ads

Breaking News
recent

TIMU YA SIMBA SPORTS CLUB KUCHUANA VIKALI NA TIMU YA "MATHARE UTD" KUTOKA KENYA.

 Asili Yetu © All rights reserved

                                       Timu ya Simba Sports Club katika mechi zilizopita.

Timu ya Simba Sports Club inatarajiwa kujitupa ndani ya uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha tarehe 26/8/2012 katika mechi ya kirafiki kati yake na timu ya Mathare Utd kutoka Kenya.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo mjini Arusha Mratibu wa mechi hiyo George Wakuganda amesema kuwa Timu ya Simba iko kambini ikijiandaa na mechi hiyo ya siku ya jumapili ya tarehe 26 mwezi huu, huku timu ya Mathare Utd kutoka Kenya kuwasili kesho 25/8/2012.

George ameeleza kuwa maandalizi yote kuhusu mechi hiyo kati ya Simba na Mathare Utd yamekwisha kamilika na kudai kuwa timu ya Simba itatumia mchezo huo kuwaonyesha mashabiki wake wote wachezaji wote wapya waliosajiriwa katika timu ya Simba kwa msimu huu wa 2012 / 2013.
Mratibu huyo amewaomba mashabiki wote kuja kushuhudia mchezo huo uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa mpira mkoani Arusha na mikoa ya jirani.

Nae Charles Mwaimu kutoka kutoka katika Chama cha Kandanda cha wilaya ya  Arusha alisema kwa uzoefu walionao katika kuaandaa mechi kubwa mkoani hapa, wamejiandaa vyema na mechi hii kati ya timu ya Simba na Mathare Utd ya Kenya.
Charles pia mefafanua kuhusu kiingilio cha mechi hiyo kuwa kwa jukwaa "A" Shilingi 10,000, Jukwaa "B" Shilingi 5,000 na Jukwaa "C" ni shilingi 3,000.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.