Header Ads

Breaking News
recent

MAISHA YA KIJIJINI HUWA NA VIJIMAMBO NA CHANGAMOTO KAMA HIZI.

All rights reserved to Asili Yetu.

Hii ni nyumba ya msonge ambayo wakazi wa kijiji cha Nyichoka mkoani mara, huitumia kulazia mifugo (Mbuzi)
Kuna aina nyingi sana za maisha, lakini kunaaina kuu mbili  za maisha, nazo ni maisha ya mjini na kijijini.Ni wazi kuwa wakazi wa mjini hutegemea  saana vijijini hasa katika swala zima la mazao. Hakuna ubishi kuwa maisha ya kijijini ni tabu tupu, hasa katika huduma za kijamii kama maji, zahanati, vyombo vya habari, elimu, miundo mbinu na vingine vingi kama imani potofu.

Ukabila nao unachukua kasi kubwa katika jamii kadhaa  huko vijijini, nikitu cha kushangaza mpaka leo makabila flani bado yanajitenga na makabila mengine, ni sawa kwasababu kila kabila lina miiko yao na tamaduni zake. Lakini wahenga walisema umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu, kisawahili ni nguzo pekee inayounganisha watu wote tokea mwaka wa 1961 wakati Tanganyika ikipata uhuru wake mpaka sasa, hivyo ni vyema watanzania tukaweka tofauti zetu pembeni na kufanya maendeleo.

Huenda leo hii ningepata nafasi ya kuulizwa ungependa nini watu wa kijijini wafanyiwe , basi ningekuwa na meengi ya kueleza, lakini hili pia ni moja wapo; ningepeda baadhi ya vipindi vya Luninga na Redio vipewe udhamini huko ndani kabisa vijijii ambako mpaka leo wananchi wanajua kuwa  Nyerere ndio rais mpaka sasa.

Hiki ni chombo maalum kilichotengenezwa kwa kutumia fito za miti kwaajiri ya kusafirishia mbolea aina ya samadi kwenda shambani.


No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.