All rights reserved to Asili Yetu.
![]() |
| Baby Madaha |
Akizungumza na na jarida la Ijumaa hivi karibuni, Baby alisema kuwa bwana wake huyo wametokea kupendana sana na wanachofikiria ni mmoja kubadili dini kumfuata mwenzake ili waweze kuoana.
Alisema kwa kuwa anampenda mwanaume huyo ambaye hapendi kumuanika hadharani, ikibidi yeye atabadili dini ili kurahisisha zoezi hilo la kuishi kama mke na mume.
“Nampenda sana na mipango yetu ni kuoana licha ya kwamba muda bado na kwa kuwa yeye ni Muislam, ikibidi mimi nitabadili dini kumfuata yeye ili lengo letu litimie,” alisema msanii huyo na kuongeza:
“Mimi naona dini zote ni sawa, kikubwa ni kumuabudu Mungu hivyo nimekubali vyovyote itakavyokuwa lakini nakula kwanza ujana ‘then’ ndiyo niolewe.”

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA