Header Ads

Breaking News
recent

ADELE, MSHINDI WA TUZO ZA GRAMMY 2011 ALIYEVUNJA REKODI

All rights reserved by Victor Machota.

Adele...Grammy Awards
Anafahamika kwa jina la Adele, yeye ndiye aliyeongoza kwa kupata tuzo sita  zaGammy kwa mwaka 2011 zilizofanyika siku ya jumapili ya mwezi huu.
Adele mwenye umri wa miaka 21 kutoka Uingereza, ambae Albam yake ya "21" iliongoza kwa mauzo kwa mwaka mzima wa 2011, ameongoza kwa kupata tuzo za Grammy kwa "Wimbo bora wa mwaka","Album bora ya mwaka" "Recor ya mwaka", "Pop Solo bora ya mwaka", "Pop Vocal Album", na "Video bora fupi ya mwaka 2011".

Katika tuzo hizo Adele alitumbuiza na wimbo wake maarufu wa "Rolling in the deep" wimbo wake wa kwanza kuperform tokea mwezi Novemba alipofanyiwa upasuaji mdogo wa koo.Tuzo za Grammy hazikuwa zina muhusu Adele tuu, bali wasanii wengipia walikuwepo na kupiga shoo kama Chris Broun,Foo Fighters na Lady Antebellum.
Kifo cha msanii Whitney Houston kilitia simanzi katika tuzo hizo, hususani msanii Jennifer Hudson alivyopanda kuperform wimbo wa "I Will Always Love You" uliomlenga msanii Whitney Houston aliyefariki siku moja kabla ya kufanyika kwa tuzo hizo.Shoo hiyo iliongozwa na rapper LL Cool J.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.