| Baadhi ya miili ya wahanga wa ajali ya meli pamoja na waokoaji wakiendelea kutoa huduma. |
| Baadhi ya wanajeshi wa kikosi cha jeshi la polisi (FFU) pamoja na wanaharakati wengine wa uokozi wakibeba majeruhi |
| Ni baadhi ya waokowaji wakiwa katika zoezi zima la uokowaji wa watoto |
| Hivi ndivyo meli ya Spice Island ilivyo pata ajali |
![]() | |
| Hawa ni baadhi ya raia wakisubili kutambua maiti ya ndugu zao |
| Meli hiyo ikionekana kuendelea kuzama taratibu |
Baadhi ya wanajeshi wa vikosi mbali mbali vya ulinzi
wakibeba majeruhi Marium Mohamed Muradi (29) kutoka Tanga,aliyenusurika na kifo
katika ajali ya kuzama kwa Meli ya Mv Spice Islander
Akitoa taarifa hiyo mbele ya vyombo vya habari leo jioni, huko Ikulu mjini Zanzibar DK Shein amesema Serikali inatangaza siku tatu za maombolezo kuanzia kesho tarehe 11 September, aidha katika kipindi hicho sherehe na tafrija zote hazina budi kusitishwa sambamba na bendera kupepea nusu mlingoti. Akielezea mikakati ya Serikali katika msiba huo amesema serikali itashughulikia kikamilifu ikiwa ni pamoja na kuwatambua waliofariki,kuwasaidia waliookolewa na waliopata maumivu, itashughulikia maziko kwa wale wote waliofariki kwa wale watakao tambuliwa. Aidha DK Shein amesema kwa wale ambao hawatatambuliwa na jamaa zao Serikali itachukua jukumu la kuwazika katiaka lililotengea huko KAMA wilaya ya Magharibi Unguja. Rais alivipongeza vikosi vya ulinzi kwa kazi nzuri waliofanya katika harakati za uokozi wakishirikiana na Wananchi, pamoja na vyombo vya habari ambavyo vimefanya kazi ya ziada ya kuwajuulisha wananchi matokeo yote ya ajali hiyo. Aliwataka wananchi wote na zaidi waliofiwa kuwa wastahamilivu kwa msiba huo uliowafika na waone kuwa hayo ni majaala ya Mwenyezi Mungu. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, mara baada ya kuzungumza na vyombo vya habari alitembelea eneo la Maisara ambapo maiti za wahanga hao wa ajali ya meli wanapofikia ili kutambuliwa na jamaa zao. Wakati huo huo mpaka hivi sasa watu wapatao 620 wameokolewa wakiwa hai na watu 189 wamefariki dunia hata hivyo hali ya uokozi inaendelea. TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUZAMA KWA MELI YA SPICE ISLANDERS Usiku wa kuamkia leo Tarehe 10/09/2011 majira ya saa 9 za usiku kumetokea ajali ya kuzama kwa meli ya MV. SPICE ISLANDERS katika bahari ya eneo la Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja. Taarifa ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud Mohamed, imesema Meli hiyo ilikuwa ikitokea Unguja kuelekea Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba ambapo Meli hiyo ilikuwa imepakia mizigo na abiria. Waziri Aboud amesema Serikali inaendelea na juhudi za kukitafuta chombo hicho pamoja na watu waliokuwemo. Amesema kwamba Serikali tayari imeshatuma vyombo vya uokozi, ulinzi na usalama katika eneo la tukio na mtakuwa mkipewa taarifa mara kwa mara. Waziri Aboud amewataka Wananchi kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu na tuendelee kusikiliza taarifa za Serikali kupitia vyombo vya habari ili kupata taarifa zaidi. IMETOLEWA NA:- IDARA YA HABARI (MAELEZO) ZANZIBAR 10/09/2011 |

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA