KUUWAWA KWA OSAMA BIN LADEN.
| NEWYORK |
| Watu walikusanyika kuangalia tukio kwenye TV |
| Majeshi kuelekea alikokuwa Osama |
| Osama Bin Laden |
Rais wa Marekani Barack Obama amethibitisha kuuwawa kwa kiongozi huyo ambaye amekuwa akitafutwa kwa kipindi kirefu sasa.Obama amesema kuwa kikosi cha oparetion hiyo kiliweza kumshambulia kiongozi huyo wa Al Qaeda Osama Bin Laden kwa kushirikiana na urinzi wa sirikali ya Pakistani ambao ndio waliongoza kikosi cha marekani kufika Abottabad kama kilimita 50 sawa na miles 30 kutoka kusini mwa mji wa Islamabad.
Mbali na mlipuko wa World Trade Centre, kiongozi huyo wa kikundi cha ugaidi alilipua ubarozi wa marekani Tanzania na kenya mwaka 1998 na 2000 kule Yemen.
Baada ya kutangazwa rasmi kwa taarifa hiyo na Rais Obama, watu walianza kukusanyika nje ya ikulu ya Marekani na kuanza kusherehekea tukio hilo ambalo Rais mstaafu wa marekani George W. Bush amesema ni kitendo cha ushujaa.
Katika tukio hilo la kumkamata kiongozi huyo wa Al Qaeda OSAMA BIN LADEN Rais Obama amethibitisha kutokuathirika na kitu chochota kwa wanajeshi wake huko Pakistani.
Mpenzi msomaji, fungua blog hii tena kwa habari za kina kuhusiana na Mauaji ya Kiongozi huyu wa Al Qaeda.
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA