Karibu mpendwa msomaji katika ukurasa mwingine wa
"Ndoto Yetu".Ukurasa unaokupa njia ya kukabiliana na changamoto za
hapa na pale zinazokukabili katika maisha yako ya kila siku. Fanya kama unaangalia hapa chini utapata nini kimejili
leo, karibu.
Wahenga walisema “penye nia pananjia” hii inaonyesha kwamba
ni njinsi gani walio wengi hushindwa kugundua njia ya kuweza kuwafikisha katika
ndoto au malengo yao, hivyo kujikuta wakipoteza nia na kushindwa kutimiza ndoto
zao.
Kugundua ni jinsi gani
unaweza kufanikisha malengo yako sii vigumu, isipokuwa unatakiwa kuwa na
subira katika malengo yako na hapo ndipo utakapo fanikiwa.
Hutakiwi kukata tamaa katika maisha, isipokuwa unatakiwa
kuweka akili na mawazo yako yote kwa kile unachokifanya, huku ukijua kuwa
niwapi unataka kufika au nini ungehitaji kupata. “If you heed this advice, and
keep your goal firmly in mind, you will find that there is away. Keep going
until you find a way that works. Even the ways that don’t work will teach you
many things.”
Kuna kitu chochote ambacho ulijaribu kufanya maishani mwako
lakini kwa muda ufupi kikaishia
njiani?.Kama ulijaribu tena na tena huenda kwa sasa umeona ni kwajinsi gani
kitu hicho ulichojaribu tena kukifanya kimeweza kubadilisha maisha yako!
Naam!! Muda haujaisha kujaribu, fanya hivyo sasa, unaweza
ukatupilia mbali ndoto au malengo uliyokwisha fanya ukashindwa, jipange na
uanze kujaribu upya, kwasababu mazuri yako mbele.
Usiwe na mategemeo ya haraka haraka kuwa ndoto au malengo
yako ya kwanza tu kufanikiwa, hata yakiwa mia moja lakini yasipokuwa na
mpangilio mzuri hayataweza kutimia kamwe. Ila tafuta njia mbadala itakayoweza
kutumika katika lengo au ndoto yako ya kwanza na siyo kubeba malengo yote kwa
wakati moja.
Malengo yaliyo makubwa huchukuwa muda mrefu kufanikiwa,
hivyo hutakiwa mwenye malengo hayo kuyarudia kwa mara nyingi, nahii hupelekea
watu wengi kushindwa kufikia malengo yao, sii kwamba wameshindwa kabisa bali
wameacha kujaribu.Wanafikiri kwamba kama jambo fulani halikufanikiwa kwa haraka
basi halitofanikiwa kamwe, “sii kweli”.
“I truly believe that there is a way to have everything you
want in life” japokuwa sii kila mara tunaweza kufikia malengo kwa haraka kama
wengi tupendavyo.Wakati mwingine ni kwasababu kile tunacho kihitaji au
kikusudia sii kile tunacho kifanya, hivyo tunahitaji muda wa kufikiri na kuweka
sawa maswala yatakayotupatia furaha maishani mwetu.
Je, umesha wahi kuwa na malengo ambayo ulikwisha kata tama
ya malengo hayo na siku moja ghafla yakatimilika bila wewe kutegemea?
Nimekuuliza hivyo makusudi kwasababu kile tunacho kihitaji hatuko tayari
kukipata, hivyo tunahitaji maandalizi hata ya kisaikolojia. “Katika hali ya
kawaida ukiwa na malengo yako wapo watu watasema anaota ndoto za Alinacha but
always ili kuwa na mafanikio unaambiwa think big,ukiwaza kupata kidogo utapata
kidogo lakini kama unawaza kikubwa basi utapata kikubwa”.
Ni kweli maisha wakati mwingine huwa magumu lakini usikate
tamaa, kaza buti, safari ya maisha ni ndefu.
TEMBELEA JITAMBUE KWANZA
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA