Header Ads

Breaking News
recent

Muigizaji mkongwe wa filamu nchini India, Shashi Kapoor amefariki dunia

Muigizaji mkongwe wa filamu nchini India, Shashi Kapoor amefariki dunia leo katika Hospitali ya Kokilaben mjini Mumbai akiwa na umri wa miaka 79.

Bw. Kapoor, alitamba na filamu maarufu kutoka Bollywood kama vile Trishul (1978), Namak Halaal(1982), Deewar (1995), Kabhie Kabhie (1976) na nyingine nyingi, amekuwa akiugua kwa muda kabla ya kukutwa na mauti siku ya jana.

Shashi anatoka katika familia ya vipaji ya Kapoor ambayo imetawala tasnia ya filamu za Kihindi kwa miongo mingi.

Katika enzi za uhai wake Kapoor alishawahi kushinda tuzo nyingi za filamu za taifa na alitunukiwa tuzo kuu ya heshima ya  Padman Bhushan inayotolewa na raia wa India mwaka 2011.

Mbali na filamu za kihindi Kapoor ameigiza pia na wasanii wengine kutoka Marekani, Uingereza na Urusi kama filamu ya Vozvrashcheniye Bagdadskogo Vora ya mwaka 1988.

Kwa mujibu wa mtandao wa Hindu Times, Kapoor amefariki kwa ugonjwa wa figo ambao ulikuwa unamsumbua kwa miaka mingi.

Tayari Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi ametoa pole kwa familia ya marehemu Kapoor kwa kutumia ukurasa wake wa Twitter.

PAKUA NYIMBO ZILIZOTOKA WIKI HII>>>DOWNLOAD
SUBSCRIBE YouTube account yetu upate video zaidi.
Kupata Update kibao, like Facebook account yetu.
Twitter Account yetu>>>Asili Yetu Tanzania
 

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.