Mwigizaji wa kike duniani aliyelipwa pesa nyingi zaidi kwa mwaka 2017.
Emma Stone ndiye mwigizaji wa kike anayelipwa pesa nyingi zaidi miongoni mwa waigizaji duniani mwaka huu.
Mwigizaji
huyo aliyeigiza katika filamu iliyovuma sana mwaka huu ya La La Land
alilipwa $26m (£20m) katika kipindi cha miezi 12 kati ya Juni 2016 na
Juni 2017, sana kutokana na ufanizi wa filamu hiyo.Malipo hayo yalimfanya kuongoza katika orodha ya kila mwaka ya jarida la Forbes, na kuwashinda Jennifer Anniston na Emma Watson.
Jennifer Lawrence, aliyeongoza 2016, alikuwa wa tatu baada ya kulipwa $24m (£19m).
Mapato ya Emma yalipanda kwa 160% ukilinganisha na mwaka 2016, alipolipwa $10m (£8m). Jennifer Lawrence alikuwa ameongoza orodha hiyo ya Forbes kwa miaka miwili iliyotangulia, sana kutokana na ufanisi wa filamu za Hunger Games.
![]() |
| Jennifer Lawrence |
Mwaka huu, waigizaji wa kike 10 wanaolipwa pesa nyingi zaidi kwa pamoja walipata $172.5m (£134m), kabla ya kutozwa ada na ushuru.
Waigizaji wa kike hao wote walipata zaidi ya $11.5m (£9m) kila mmoja.
Jennifer Aniston alikuwa wa pili baada ya kupata $25.5m (£20m), sana kutokana na kutumiwa kwake kuuza Smartwater, mafuta ya ngozi ya Aveeno na shirika la ndege la Emirates.
Emma Watson ndiye Mwingereza pekee aliyekuwa kwenye orodha hiyo ya 10 bora, akiwa katika nafasi ya sita.
Waigizaji hao wengine walikuwa ni Melissa McCarthy, Mila Kunis, Charlize Theron, Cate Blanchett, Julia Roberts na Amy Adams.
Mwaka uliopita, waigizaji wa kike 10 waliolipwa pesa nyingi zaidi Hollywood walilipwa $205m (£159m) kwa pamoja - kiasi cha chini sana ukilinganishwa na waigizaji 10 wa juu zaidi wa kiume.




No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA