Ujio wa Sanjay Dutty 'Star wa filamu za Kihindi' umekuwa gumzo Tanzania.
Magazeti, Redio, Tv na mitandao ya kijamii vimeonekana kumzungumzia muigizaji mkongwe na anayefanya vizuri kwenye soko la filamu India,
Sanjay Balraj Dutt, aliyekuja nchini kwa ajili ya mapumziko anatarajiwa
kudumu kwa siku 21 ambapo atatembelea mbuga za wanyama na vivutio mbali
mbali vilivyopo nchini.
Sanjay Dutt amefika Arusha mapema jana akitokea Dar es salaam kwa ajili ya kuzuru mbuga za wanyama, Ngorongoro, Serengeti, mbuga ya Selou na vivutio vingine vilivyopo nchini.
Chanzo: Eatv
Ujio wa Sanjay
Dutt umethibitishwa na mwenyeji wake ambaye ni Mbunge wa Manonga, Seif
Gulamali ambaye amesema uwepo wa msanii huyo ni kipimo cha kuwa sekta ya
utalii nchini inaendelea kupanuka.
![]() |
Muigizaji Sanjay Dutt (kushoto) akipeana mkono na Mbunge Gulamali |
"Uwepo wa Sanjay Dutt nchini
ni fursa kubwa sana.Wahusika wa utalii hapa nchini wakiona
fursa katika kuutangaza zaidi utalii wetu ni vyema pia wakamtumia kwani
mtu huyu ni mkubwa sana kwenye sanaa ya filamu.
Lakini pia kuja kwake hapa nchini ni wazi tunazidi kukua kwenye sekta hii, na tutapata mapato kupitia kuwepo kwake kwani atakuwepo kwa takribani siku 21" alisema Mhe. Gulamali
Hata hivyo mbunge huyo amewataka waigizaji wa
filamu nchini kuchangamkia fursa ya kukutana na muigizaji huyo kwa
ajili ya kupata madini yatakayowasaidia kukuza na kupanua soko la
filamu.Lakini pia kuja kwake hapa nchini ni wazi tunazidi kukua kwenye sekta hii, na tutapata mapato kupitia kuwepo kwake kwani atakuwepo kwa takribani siku 21" alisema Mhe. Gulamali
Sanjay Dutt amefika Arusha mapema jana akitokea Dar es salaam kwa ajili ya kuzuru mbuga za wanyama, Ngorongoro, Serengeti, mbuga ya Selou na vivutio vingine vilivyopo nchini.
Chanzo: Eatv
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA