Sunday, May 18 2025

Header Ads

Mfuko wenye vumbi na mawe kutoka Mwezini wapigwa mnada Marekani.

Mfuko moja uliotumika na mwananga Neil Amstrong kukusanya violezi vya mwezi, umeuzwa kwa dola milioni 1.8 mjini New York.
 
Mfuko huo katika chombo cha angani cha Apolo 11 mwaka 1969 ulinunuliwa katika eneo la Sotheyby na mtu asiyejulikana.
 
Mfuko huo bado una vumbi na mawe madogo madogo kutoka mwezini.
 
Mnada huo unajiri baada ya mapambano mahakamani kuhusu umiliki wa kifaa hicho cha kipekee kutoka Apollo 11 ambao ulikuwa katika mikono ya mtu binafsi.
 
Baada ya chombo hicho cha angani kurudi duniani, vifaa vyote vilipelekwa katika jumba la makumbusho la Smithsonian.
 
Hatahivyo mfuko huo uliachwa katika boksi katika kituo cha vyombo vya angani cha Johnson kutokana na makosa ya kihesabu.
 
Baadaye haukutambulika wakati wa mnada wa serikali, ukiuzwa kwa dola 995 pekee kwa wakili mmoja wa Illinois 2015.
 
Hatahivyo mamlaka inayosimamia vyombo vya angani Nasa ilijarabu kuuchukua mfuko huo, lakini mapema mwaka huu, jaji mmoja aliamuru kwamba, ulimilikiwa na mnunuzi huyo kimakosa ambaye baadaye ailiupeleka katika mnada huo wa Sutheby.
Chanzo: BBC

Leave a Comment

Powered by Blogger.