Daraja linalokisiwa kuwa refu zaidi duniani lazinduliwa nchini Uswizi
Daraja lililotundikwa lenye mita 500 linalokisiwa kuwa refu zaidi duniani limefunguliwa katika mji wa Zermatt nchini Uswizi.
Bodi za utalii ya Zermatt inasema kuwa ndio daraja refu zaidi duniani ,ijapokuwa daraja la mita 405 mjini Reutte Austria limetundikwa mita 110 juu kutoka ardhini.
Daraja hilo linachukua mahala pa daraja jingine ambalo lilikuwa limeharibiwa na mwamba.
Daraja hilo jipya ambalo ambalo lina uzito wa tani nane limewekwa kifaa cha ambacho linalizuia kuyumbayumba ,kulingana na bodi ya watalii ya Zermatt.
Daraja hilo lipo kati ya Zermatt na Grachen kusini mwa Switzerland.
Stori na BBC



No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA