Orodha ya vyuo vikuu bora duniani kote kwa mwaka 2017.
Orodha mpya ya kila mwaka ya vyuo
vikuu bora zaidi duniani imetangazwa, ambapo chuo kikuu cha
Massachusetts Institute of Technology (MIT) cha Marekani bado
kinaongoza.
Orodha hiyo ilishirikisha vyuo vikuu karibu 1,000.
Vyuo vikuu hupimwa kwa mambo kama vile majarida na vitabu vya kisomi vilivyochapishwa, makala zilizonukuliwa, maoni ya wasomi pamoja na waajiri na pia ushiriki wa vyuo vikuu hivyo katika ngazi ya kimataifa.
Chuo kikuu cha Nairobi kimeorodheshwa kuwa kati ya nambari 801 na nambari 1000, kutoka kuanzia nambari 701 hadi 1000mwaka jana, sawa na Chuo Kikuu cha Makerere.
Vyuo vikuu 10 bora zaidi duniani kwa mujibu wa QS World University Rankings
- Massachusetts Institute of Technology (MIT)
- Stanford
- Harvard
- California Institute of Technology (Caltech)
- Cambridge
- Oxford
- University College London
- Imperial College London
- Chicago
- ETH Zurich
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA