Fahamu gari lenye kasi zaidi duniani kwa mwaka 2017.
Gari lenye
mwendo wa kasi zaidi duniani litakimbia kwa mara ya kwanza kabisa tarehe 26 mwezi
Oktoba.
Gari hilo litakimbia kwa kasi ya chini wakati wa majiribio kwenye uwanja wa ndege wa Newquay huko
Conawall.
Wahandisi
wanataka kukagua mitambo yote ya gari hilo kabla ya kulipeleka nchini Afrika
Kusini mwaka ujao, kukimbia kuvunja rekodi ya mbio ya kasi zaidi ardhini.
Kwa sasa
rekodi ya kasi ardhini
ni 763mph au 1,228km/h, na gai hilo linalofahamika kama Bloodhound litaongeza kasi kwanza hadi 800mph na
kisha 1000mph.
Majaribio ya
Newquay hayatafikia kasi kama hiyo kwa kuwa barabara ya mita 2,744 ni fupi kiliwezesha Bloodhound kushika
kasi.
Badala yake
dereva Andy
Greren, ataliendesha gari hilo kwa kasi ya 200mph likitumia injini ya ndege
aina ya Eurofighter-Typhoon
Itakua siku
ngumu kwa Dereva Andy Green kwa sababu itakuwa mara yake ya kwanza kuliendesha
gari hilo.
Matarajio ni
kuwa Bloodhound
litapelekwa eneo la Hakskeen Pan huko Northen Cape nchini Afrika Kusini
kwa muda wa mwaka mmoja hivi unaokuja kajaribu kutimiza lengo lake.
Ili hilo
liweze kufanyika, awamu nyingine ya uundaji wa roketi hiyo ni lazima ukamilike.
Na bbc
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA