Orodha ya wanamuziki 19 matajiri nchini Uingereza.
Ziara ya ulimwengu na mauzo ya
baadhi ya albamu yalimpatia msanii Adele kitita cha pauni milioni 40
mwaka uliopita, kulingana na orodha ya wanamuziki tajiri ya gazeti la
Sunday Times.
Mwanamuziki huyo wa muziki wa Pop aliongeza utajiri
wake kutoka pauni milioni 85 hadi pauni milioni 125 ikimaanisha ndiye
mwanamuziki tajiri zaidi wa kike katika gazeti hilo linaloangaiza
utajiri wa wanamuziki kila mwaka.
Hatahivyo ameshikilia nafasi ya 19 pamoja na mwanamuziki mwengine wa kiume katika oroadha ya wanamuziki matajiri nchini Uingereza ambayo imetawaliwa na wanamuziki wa kiume.
Paul Mc Cartney anaongoza orodha hiyo akiwa na pauni milioni 780 pamoja na mkewe.
Wanafuatwa na West End Mogul Lord Lioyd Webber, U2, Sir Elton John, Sir Mick Jagger na mpiga bendi mwenza wa Rolling stones Keith Richards.
Adele anashikilia nafasi ya 19 akiwa na pauni milioni 125 pamoja na mpiga gita wa Queen Brian May.
Kuongezeka kwa utajiri wake kunadaiwa kutokana na ziara 122 za ulimwenguni ambazo zilimpatia kitita cha pauni milioni 138 mbali na ufanisi wake wa albamu yake ya tatu 25 ambayo iliuza kopi 2.4 duniani 2016.

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA