Dawa ya magonjwa sugu na yenye nguvu mara elfu moja zaidi yagunduliwa nchini Marekani.
Wanasayansi nchini Marekani
wamefanikiwa kupambana na maradhi yaliyokuwa sugu kwa dawa za kupambana
na vijidudu yaani antibiotics tatizo ambalo lilikuwa tishio dhidi ya
sekta ya afya duniani.
Vancomycin ilikuwa ikipoteza uwezo wake wa kupambana na bacteria aitwae enterococci ambaye husabisha madhara kwenye njia ya haja ndogo na vidonda.
Aina mpya ya dawa hii ina nguvu mara elfu moja zaidi na hushambulia vijidudu kwa njia tatu tofauti, kiasi cha vijidudu kushindwa kupambana na dawa hiyo.
Inakadiriwa kuwa vijidudu vilivyokuwa vikipambana na dawa za antibiotics husababisha vifo takriban elfu hamsini kila mwaka nchini Marekani na barani Ulaya.
Stori na BBC
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA