Almas mbili zilizovunja rekodi ya dunia kwa bei.
Vipuli viwili vya almasi, vimevunja
rekodi ya dunia kwa kuuzwa kwa kiwango kikubwa zaidi cha pesa, cha
takriban dola milioni 58, katika soko la mnada nchini Uswizi.
Viliuzwa tofauti tofauti lakini vikanunuliwa na mnunuzi mmoja.
Kulikuwa na wasiwasi kwamba vipuli hivyo, vinavyojulikana kama Apollo na Artemis havitakuwa pamoja baada ya kupigwa mnada mjini Geneva.
Viliuzwa tofauti kwa sababu almasi za buluu ni nadra ukilinganisha na zile za rangi ra waridi.
Hata ijapkuwa ziliuzwa tofauti lakini vitasalia kuwa pamoja baada ya kupata mnunuzi mmoja.
Alamasi ya Apollo yenye rangi ya buluu iliuzwa kwa takriban dola milioni 42 huku Artemis yenye rangi ya waridi ikiuzwa kwa dola milioni 15.5.
Na BBC
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA