Utafiti: Baadhi ya Betri zitumikazo katika simu zasemekana kuwa na sumu.
Zaidi
ya gesi 100 zinazoweza kusababisha kifo hutolewa na betri
zinazopatikana miongoni mwa mabilioni ya vifaa vinavyotumiwa na raia
wengi duniani kama vile simu aina ya smartphone na vipatakilishi
kulingana na utafiti mpya.
Utafiti
huo ulibaini gesi 100 zenye sumu zinazotolewa na betri za Lithium,
ikiwemo ile ya kaboni monoksaidi, ambayo inaweza kusababisha kujikuna
katika ngozi, macho na pua mbali na kuathiri mazingira.
Watafiti
kutoka taasisi ya ulinzi ya NBC nchini Marekani pamoja na chuo kikuu cha
Tsinghua nchini China wamesema kuwa watu wengi huenda hawajui hatari ya
betri kupata moto, kuharibika ama kutumia chaji isiofaa katika vifaa
hivyo, jarida la Science Explorer limeripoti.
Katika utafiti
huo mpya,walichunguza betri moja ya kuchaji inayojulikana kama
Lithium-ion,ambayo huwekwa katika vifaa vinavyotumika kila mwaka.
Sun na wenzake waligundua sababu kadhaa ambazo zinaweza kuongeza gesi zenye sumu zinazotolewa.
Betri zilizopata chaji zaidi hutoa gesi zaidi za sumu ikilinganishwa na betri ilio na asilimia 50 ya chaji.
Source: bbc-swahili

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA