Justin Bieber ashuka jukwaani kwa hasira, sababu kelele za mashabiki.
Stori zinatoka kwa Justin Bieber wakwetu, hii ni baada ya kuondoka katika
jukwaa la tamasha lake mjini Manchester baada ya kuwataka mashabiki
kutopiga kelele wakati anapoimba.
Wakati wa matamasha yake matatu yalizopita katika mji huo ikiwa ni miongoni mwa ziara yake ya dunia nzima, mwanamuziki huyo alisema : "Nathamini msaada ninaopata, nathamini mapenzi mnayonipa na nathamini ukarimu wenu. Lakini kelele mnazopiga wakati ninapoimba lazima zisitishwe.Tafadhali na ahsanteni.Sidhani ni muhimu ninapojaribu kusema kitu na nyinyi mnapiga kelele.
Kwa upande wa mashabiki walipokataa kusitisha kelele zao, Bieber aliangusha kipaza sauti na kuondoka katika jukwaa, huku baadhi ya mashabiki wakimzomea.
Baadaye mkali huyo wa miaka 22 alirudi kuendelea na tamasha lake na kuelezea kwa nini aliondoka kwa hasira.
''Nahisi kwamba nataka kuwasiliana nanyi.Lengo hapa ni ninapowaangalia katika macho, mnajua kwamba tuko katika wakati muhimu na kwamba tunawasiliana''.

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA