Faida za kulima Mboga Mboga katika maisha ya sasa.
Katika maisha ya familia ni lazima
kujituma katika mambo yanayowezekana angalau kupunguza gharama za maisha
yanayoikabili familia. Leo tumeona ni vyema tukafahamu mambo muhimu
tunayoyapuuza, lakini yanaweza kusaidia kupunguza ukali wa maisha.
Kilimo cha mboga mboga ndani ya familia
ni hatua pekee ya kupunguza ukali wa maisha na kuepuka gharama zisizo za msingi
ndani ya familia.
Hapa nazunguzia kwa wale wenye maeneo binafsi na wanaishi mjini au hata vijijini, tumia eneo ulilonalo kulima hata matuta mawili tu ya mboga mboga; kwamfano nyanya, sukuma wiki, mchicha na kadhalika.
Hapa nazunguzia kwa wale wenye maeneo binafsi na wanaishi mjini au hata vijijini, tumia eneo ulilonalo kulima hata matuta mawili tu ya mboga mboga; kwamfano nyanya, sukuma wiki, mchicha na kadhalika.
Tumia nafasi ulionayo hata kama ni
kutumia makopo kama mauwa, panga miche yako ya nyanya na sukuma wiki au
mchicha, ili kuokoa pesa yako kwenda sokoni kila siku. Kuna baadhi ya mboga mboga
huchukuwa siku chache kuota na kukua; kwamfano mchicha huchukuwa siku chache
tayari unavunwa.
Kuwa na bustani ndogo ya mboga mboga
nyumbani haikushushi hadhi hata kama wewe ni tajiri, unaweza kumpa maelekezo
msaidizi wako pale nyumbani akapanda hata matuta mawili tuu ya karoti au
nyanya, endapo wewe uko bize.
Bustani ya mboga mboga katika ngazi ya
familia sio tuu inasaidia kupunguza matumizi bari inakupatia uzoefu wa kujituma
katika kazi.
Kwamfano wenzetu wa majuu hutenga muda wao wa jioni na asubuhi sana
kufanya kitu katika bustani zao aidha za maua au mboga mboga.
Kama bado hukujua
utamu wa bustani, basi anza leo.
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA