Sayansi Na Teknolojia: Ndege ndefu zaidi hatimaye yaruka nchini Uingereza.
Safari ya ndege ndefu zaidi dunian imeanza nchini Uingereza baada ya majaribio ya awali kufutwa dakika za mwisho.
Ndege hiyo hairuhusiwi kuruka usiku inapofanyiwa majaribio. Ndege hii iliundwa kwanza kwa serikali ya Marekani kama ndege ya kufanya ujasusi lakini mradi huo ukafutwa kutokana na ukosefu wa fedha.
Kisha kampuni ya uingereza ya Hybrid Air Vehicles (HAV) ikazindua kampeni ya kufanikisha mradi huo.
Ndege hiyo ina uwezo wa kusalia angani kwa takriban siku tano.
Kampuni ya HAV inasema ndege hiyo itatumiwa kwa masuala kadhj yakiwemo ujasusi, mawasiliano, kusafirisha misaada na hata abiria.
CHANZO: BBC


No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA