Ndege ndefu zadi duniani yapata ajali ikiwa katika majaribio ya pili angani.
Ndege ndefu zaidi duniani - Airlander 10 - imeharibika baada ya kuanguka ikitua kwenye safari yake ya pili ya kufanyiwa majaribio.
Ndege
hiyo ya urefu wa 302ft (92m) - ambayo kwa kiasi fulani ni ndege na pia
kwa kiasi fulani puto - iliharibika ikiwa katika uwanja wa Cardington,
Bedfordshire nchini Uingereza.Ndege hiyo ya thamani ya £25m imeharibika eneo wanamoketi marubani baada ya kuangika kwa 'pua' mwendo wa saa tano saa za Uingereza.
Airlander 10 kwa takwimu
- 44,100 lbs (20,000kg): Uzani wa ndege hiyo
- 20,000ft (6,100m): Umbali ambao inaweza kupaa juu angani
- 80 knots (148km/h): Kasi yake ya juu zaidi
- Siku 5: Muda ambao inaweza kukaa angani
- 22,050 lbs (10,000kg): Uzani ambao inaweza kubeba

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA