PROF JAY (Joseph Haule): HISTORIA YAKE YA MUZIKI IKO HAPA "ASILI YETU TANZANIA".
Joseph Haule (amezaliwa tar. 29 Desemba1975) ni msanii wa
muziki wa hip hop kutoka nchini Tanzania. Anafahamika zaidi kwa jina lake la
kisanii kama Professor Jay. Katika Tanzania, Prof. Jay anatazamika kama msanii
aliyeweza kuwateka wazee waweze kusikiliza muziki wa Bongo Flava. Hasa kwa
kibao alichofanya wakati yupo na kundi la Hard Blasters Crew – Chemsha Bongo.
Professor Jay anatokea kundi la Hard Blasters Crew. Kundi hili ni moja ya
makundi yaliyofanya muziki huu ambao hujulikana kama ‘muziki wa kizazi kipya’
kukubaliwa na sehemu kubwa ya wa Tanzania.
Maisha ya muziki
Professor Jay alianza shughuli za muziki mnamo miaka ya 90
hivi na alijiunga na kundi la ‘Hard Blasters Crew‘(HBC) mnamo mwaka 1994. Mwaka
1995 Jay na HBC walishinda kuwa kundi bora la Hip Hop nchini Tanzania. Jay na
HBC walitoa albamu ya kwanza iitwayo ‘Funaga Kazi’ mwaka 2000 Albamu hiyo
inaaminika kwamba ilileta mapinduzi makubwa sana ya muziki wa Hip Hop nchini
Tanzania. Albamu hii yenye ujumbe mzito ina nyimbo kama ‘Chemsha Bongo’ na
‘Mamsapu’ ambazo zilichangia kufanya muziki wa ‘Bongo Flava‘ kuwa wa kila rika
na kupewa heshima. Kabla ya hapo muziki huu ulionekana kuwa ni muziki wa wahuni
Msanii Binafsi.
Professor Jay aliamua kuwa msanii binafsi mnamo 2001 na muda
mfupi baada ya hapo akatoa albamu yake ya kwanza iitwayo “Machozi Jasho na
Damu”. Albamu hii ilivuma haraka sana na kumfanya Prof. Jay kupata tuzo ya kuwa
mtunzi bora wa Hip Hop nchini Tanzania kwa nyimbo yake ya ‘Ndio Mzee’ kutoka
kwenye albamu hiyo. na ikifuatiwa na Nyimbo ya “Piga Makofi na Bongo Dar es
Salaam“
Mwaka 2003 Alitoa albamu ya pili iitwayo “Mapinduzi Halisi”
ambayo nayo ilishinda tuzo ya Kili Music Awards kuwa albamu bora ya Muziki wa
Hip Hop nchini Tanzania kwa mwaka 2003. Albamu hii imebebanNyimbo kama “Zali la
Mentali”, “Msinitenge,” na “Promota Anabeep”
Mwaka 2006 Januari alitoa albamu ya tatu iliyoitwa
“J.O.S.EP.P.H”. Jina la albamu hii lilitokana na nyimbo iliyotoka Mwanzo kabla
ya Albamu kutoka. Nyimbo hii ilichaguliwa kuwa nyimbo bora ya Bongo Flava
kwenye BBC na Radio One Awards.
Mpya imewahi kuteuliwa kuwa ni albamu bora ya Hip Hop ,
Mtunzi bora wa nyimbo za Hip Hop, na Nyimbo bora ya Hip Hop ya mwaka kwenye
Kili Music Awards. 2006.”Nikusaidieje”. na Baadae Kisima Music Awards ya Kenya
ilikuwa Nyimbo bora ya Hip Hop na Video bora ya Hip Hop kutoka nchini Tanzania.
Albamu
Aluta Continua ( 2007 )
J.O.S.E.P.H. ( 2006 )
Mapinduzi Halisi ( 2003 )
MachoziJasho na Damu ( 2001 )
Imeandaliwa na DJCHOKA MUSIC
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA