Header Ads

Breaking News
recent

TAMTHILIA YA "HER MOTHER'S DAUGHTER" (Episode ya 60) SIRI YAFICHUKA DIEGO NI MTOTO WA THERESA.

Celyn
Baada ya Margaux na Celyn kugundua kuwa ni watoto wa baba mmoja, mambo yamekuwa yakimwendea Beatrice vibaya, kwani Julio amemzilia na huenda akadai taraka.

Margaux baada ya kubanwa sana na mama yake Beatrice, kwa hasira Margaux aamua kuhama na kwenda kuishi hotelini, lakini huko nako anamkuta Theresa ambaye ndiye mama yake wa kuzaa. Theresa nae anaonekana kutaka mazungumzo na Margaux ili apate kumzoea, lakini Margaux anaona ni kama kero na kuamua kwenda bar ili kumkwepa.

Lakini wakati aliporudi alimkuta Theresa akiwa amelala mlangoni akimsubiri, Margaux anaamua kumuamsha na kuendelea kumthibitishia kuwa anapoteza muda wake kumfatilia kwani yeye si mama yake.

Liam akiwa ofisini ausiku akimsubiri Celyn, alisinzia kwenye kochi na kumuacha Celyn akiwa nachapa kazi mwenyewe, baada ya hapo waliondoka na Liam kumpitisha Celyn kwao. Liam akiwa njiani akirejea nyumbani alipigiwa simu na Margaux akimuomba Liam afike pale alipo.

Margau alikuwa juu kabisa ya ghorofa akilia kwani alitaka kujitupa kwa kile alichodai kuwa anaonekana kutengwa na watu. Liam alifika pale na kupigwa na butwaa kwani Margaux alikuwa sehemu hatari sana.

Liam anafanya jitihada za kumbembeleza Margaux hadi akakubali kushuka chini na kumpa mkono, lakini pia Ethan alikuwa akimtafuta Margaux wakati alipomuacha Club na kuondoka kwenda nyumbani.

Siri yafichuka kuwa Diego ambaye jina lake la zamani ni Joshua ni mtoto wa Theresa, huenda nae alikuwa wa kuasili au wa kuzaa. Baba yake Diego ndo yule yuko Jela. Diego nae tayari anaonekana kuwa na hasira na Theresa, adai atalipiza kisasi cha kumtelekeza kwa miaka mingi.

Fuatilia dondoo zijazo hapa hapa ASILI YETU TANZANIA.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.