TAMTHILIA YA HER MOTHER'S DAUGHTER (Episode ya 59) BEATRICE ASUSIWA NA KILA MTU.
![]() |
| Celyn |
Beatrice siku za nyuma alikuwa ni mbabe sana hasa pale utakapowazungumzia wanawe, kiasi kwamba Julio alionekana kama hana sauti ndani ya nyumba. Timbili lilikuwa hivi, Beatrice alimficha Julio kuwa mtoto alipewa na Oscar wakati amemuasili Margaux akiwa mdogo.
Baada ya Oscar kusema kuwa alimlipa pesa na kumlazimisha ampatie mtoto, ndipo Julio alikasilishwa na kitendo hicho cha kumficha siri kwa muda mrefu, na hasa kitendo cha kumfanya Margaux aishi maisha ya kujua kwamba hana wazazi.
Margaux naye anaonekana kumzilia mama yake Beatrice, na kumwambia kuwa "ningepewa nafasi ya kuchagua mama nisingekuchagua wewe". Beatrice anakasilishwa sana na tamko hilo la Margaux, hivyo anamzuia asitoke nje, lakini Margaux anampuuza na kwenda zake club.
Margaux akiwa zake Club alimuona Ethern na kumuita "Ethan njoo ujumuike na mimi" Ethan alimfuata na kumpa kampani, lakini kumbe walikuwa wamekwisha zungumza na Teresa ambaye ni mama mpya wa Margaux, mara Teresa akafika pale na kumtaka Margaux aache kunywa, lakini Margaux bado hajamkubali Teresa.
Hivyo alinyanyuka na kuanza kuondoka, kwa bahati mbaya alikuwa amelewa hivyo aliyumba na kuanguka. Ethan na Teresa walimnyanyua na kumpeleka katika hoteli anakoishi Teresa na kumlaza chumbani. Teresa alimkanda na maji, je Margaux akiamka nini kitatokea?
Teresa anaanza kumkumbuka mtoto wake wa kiume wakwanza kumasili ambaye alionekana akinyang'anywa na mtu mmoja ambaye yuko jela, huenda mtoto huyo ambaye sasa atakuwa ni mtu mzima, Je atakuwa nani?
Julio je ataendelea kumliza Beatrice kama anavyozidi kufanya? Je Margaux atamkubali Beatrice au Teresa? Fuatilia dondoo zijazo hapa hapa Asili Yetu Tz.

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA