MAPENZI YA CELYN NA LIAM YATAWALA KATIKA TAMTHILIA YA "HER MOTHER'S DAUGHTER" (Episode ya 62,63 & 64).
Baada ya uvamizi wa Diego katika nyumba ya Margaux na kuharibu haribu samani za nyumba, baba yake naye arejea uraiani baada ya kufungwa magereza kwa miaka mingi tokea Diego akiwa mdogo.
Baba yake Diego naye anaonekana kuwa na chuki katika familia ya Theresa, hivyo anamsisitiza Diego kufanya kila njia ili familia ya Theresa itaabike. Baba huyo tayari ameanza kunyemelea kila wakati katika nyumba ya Theresa. Lakini pia kwa bahati nzuri Celyn tayari naye amekwisha anza kuwashitukia Diego na baba yake, ingawa hajui kuwa kama wote wawili wanamahusiano ya kiundugu.
Diego anaendelea kulipiza kisasi katika familia ya Theresa, wakati huu ameamua kutoboa matairi ya gari ya Margaux na baadaye kujitokeza na kuipeleka katika garage yake. Lakini pia Ethan ameanza kumshitukia Diego kwa vitendo vyake, kwani aliona kile kisu ambacho kilitumika kutoborea tairi ya gari la Margaux.
Baada ya Liam kutishia kuwa anakwenda nje ya nchi kwa miezi mitatu kwani alituma maombi ya kazi huko, Celyn alionekana kujutia kitendo cha kumkatalia Liam katika swala zima la mahusiano, hivyo aliwaza na kujikuta akidondosha machozi.
Siku ya safari kwa Liam iliwadia, lakini Celyn pia alifahamu kabisa Liam anaondoka katika uwanja wa ndege, hivyo alifanya jitihada hadi kuingia sehemu ya wasafiri, lakini cha kushangaza aliambiwa ndege ilikwisha ondoka, hivyo alikaa pale kwa muda huku akijiongelea. Ghafla aliamua kuondoka lakini ile anageuka tu alijikuta akijikwaa na kukuta akidakwa na Liam.
Kitendo hicho kilimfanya alainike na kumtamkia Liam neno "NAKUPENDA" Liam hakuamini, alitaka tena kusikia alimuuliza tena "unasema?" Celyn akajibu tena "NAKUPENDA", wakakumbatiana pale na kutokomea. Tokea hapo Liam na Celyn ni wapenzi wa wazi wazi kwani familia yote imekwisha jua na hata Margaux naye amekwisha fahamu japo bado hajakubaliana na hilo swala.
Ethan anafanya juhudi mbali mbali za kunasa penzi la Margaux, lakini bado juhudi zinagonga mwamba, kutokana na Margaux kutokuwa na wakati mzuri wa kufanya maamuzi.
Kesi ya Beatrice dhidi ya Zacharis sasa yafikia pabaya kwani tayari mzee Zacharis ametupwa jela, kila mmoja anaonesha kutopenda kitendo hicho cha Beatrice na baba yake kumtupa jela mzee wa watu. Celyn na mama yake Theresa wanalia kwa uchungu sana, Yolanda naye anaonyeshwa kukerwa sana na kuamua kuondoka.
DONDOO ZIJAZO:
Baada ya Zacharis kutupwa jela, Lucas amuajili baba yake Diego kuanza kufanya unyama mwingine, je safari hii atafanyiwa nani? Je penzi la Liam na Celyn litadumu? Margaux naye atafanya maamuzi gani dhidi ya mama yake Beatrice? Je Diego baada ya kuvunja flemu ya picha ya Celyn na Celyn mwenyewe kumkuta je Ceyln atatoboa siri ya kile anachokiona kwa Diego na baba yake ambaye ni hatari?

Karibu sana Asili Yetu Tanzania Blog kwa dondoo zijazo..
.jpg)
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA