 |
| Mkurugenzi wa Holili Youth Athletics Club bw. Domician Genand akihojiwa na Victor Machota. |
Akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za
Arusha Media, baada ya kumkabidhi mratibu wa mbio za Sokoine bwana Wilhelm Gidabuday, udhamini wa takribani namba 1000 zitakazotumika na wanariadha watakaoshiriki mbio za maadhimisho ya miaka 30 ya Hayati Edward Moringe Sokoine tarehe 12/4/2014 huko Monduli, Mkurugenzi huyo wa Club ya Riadha ya "Holili Youth Athletics, bwana Dominician R. Genand amesema kuwa ametoa udhamini huo baada ya kuguswa na "Utaifa Kwanza".
SIKILIZA HAPO CHINI MAHOJIANO YOTE YALIYOFANYWA NA ASILI YETU TANZANIA BLOG.
 |
| Kutoka kushoto ni mwanariadha Phaustin Baha, akifuatiwa na Domician Genand (Mkurugenzi Holili), Mwandishi wa habari na mwisho ni Gidabuday (Mratibu Sokoine Marathon). |
Hapa ni baada ya makabidhiano ya udhamini wa namba zitakazotumika na wanariadha watakaoshiriki Sokoine Mini Marathoni itakayofanyika kitaifa Monduli tarehe 12 mwezi wa nne mwaka huu, ambapo Mh. Dr Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi wa tukio hilo. SIKILIZA HAPO CHINI MAHOJIANO YOTE NA ASILI YETU TANZANIA BLOG.
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA