Header Ads

Breaking News
recent

HOTUBA YA RAIS KIKWETE KATIKA UZINDUZI WA BUNGE MAALUM LA KATIBA, HATIMAE AWEKA MAMBO WAZI.


Katika Hotuba yake iliyofuatiliwa na wengi katika historia ya utazamaji wa televisheni, rais Kikwete ameonyesha kutoegemea upande wowote japo alikiri kuwa na haki ya kutoa mawazo yake.

Wengi wamefurahia uthubutu wake wa kutoegemea upande wowote japo kwa mbali sana hisia zake ziliweza kudhihirika. Amesisitiza “Maridhiano” ndiyo yatakayowapatia watanzania katiba bora.

Hata hivyo makofi yaliweza kusikika kwa wingi kila alipoweza kuelezea changamoto za muundo wa serikali tatu; kitendo kinachoashiria kwamba wanaopenda serikali mbili pia wapo, japokuwa bila maridhiano hawataweza kupata ‘Absolute Majority” vivyo hivyo hata wale wafuasi wa serikali tatu nao watahitaji ‘Political Compromise’ 

Ndoto ya watanzania tuliowengi ni kupata Katiba iliyo bora, isiyo na ubaguzi katika pande zote, isiyo ya maslahi ya kundi flani na inayozingatia hali ya maisha ya watanzania wote yani wa hali ya juu na hali ya chini pia.

Rais amekuwa akiwasisitiza wajumbe wa kuunda katiba, kuwa makini katika utendaji wao bila kujali chama, kabila wala itikadi binafsi katika swala zima la uundaji wa Katiba mpya. Binafsi nalitakia Bunge maalum la kuunda Katiba "kila laheri" katika uundaji wa Katiba mpya itakayo tufaa watanzania wote.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.