Header Ads

Breaking News
recent

HER MOTHER'S DAUGHTER (episode ya 53 & 54) CELYN APANDISHWA CHEO HUKU MARGAUX AANZA KUWASAKA WAZAZI WAKE.

Mikanganyiko mingi imekuwa ikiwatokea wasichana Celyn na Margaux, hili likionekana kupungua makali basi linaibuka jingine. Lakini Safari hii Celyn ameonekana kung'ara katika kampuni ya Memorata baada ya juhudi zake kuzaa matunda.

Hatimae Liam amueleza tena Celyn kuhus hisia zake juu yake, lakini pia Celyn naye ashindwa kujizuia apasuajipu, atoa sababu zilizomfanya akatize urafiki wake kwa Liam. Sasa ni hivi, baada ya Celyn kumueleza ukweli Liam kuwa ni mtoto wakambo, mama yake Liam alimchukia sana Celyn na kuamua kumpiga biti Liam asionane tena na Celyn.

Lakini pia Liam hakupenda kumuona Celyn akichukuliwa na Ethan, hivyo ilibidi aondoke bila kumuaga Celyn, hapo ndipo urafiki uliingia dosali kati ya Celyn na Liam. Lakini bado moyo wa Celyn umekuwa mgumu kurudiana na Liam.

Kwa upande wa Margaux mambo yanamwendea kombo baada ya mama yake yani Beatrice kumtangaza Celyn kuwa ni mmoja wa familia yao, ambapo kisheria itakuwa baada ya siku chache tu. Baada ya sherehe hiyo siku iliyofuta Margaux alimfuata Celyn na kuanza kumpa vitisho, lakini Celyn safari hii hakuteteleka, alimueleza kuwa yeye ndiye mtoto halisi wa Julio na Margaux ni wakuasiliwa tu.

Lakini pia kutokana na juhudi za Celyn kitengo chake kilifanya vizuri katika mauzo, hivyo bodi ya Memorata ilimteuwa Celyn kuwa makamu wa Rais kitengo cha mauzo ya Memorata (hivyo ni mtu mkubwa sana katika kampuni). Hivyo katika mvutano wa Margaux, Celyn alimwambia Margaux kuwa akicheza atamtimua kazi kwani yeye ni boss wake sasa.

Margaux baaada ya kuona kuwa umaarufu wake unatoweka taratibu, akaamua kutoka ofisini akilia, lakini kwa bahati nzuri Ethan naye alikuwa akimtegea hapo nje. Margaux huwezi amini alimkumbatia Ethan na kulala kifuani huku akitokwa na machozi kama chem chemi vile.

Baada ya hapo Margaux ameamua kuomba likizo ili akawatafute wazazi wake ili nae aitulize nafsi yake kama Celyn alivyofanya. Japo mama yake yani Beatrice hataki jambo hilo la yeye kuanza kuwatafuta wazazi wake.

Katika upande wa Teresa mama yake Celyn, kumbuka wanasoma chuo kimoja na Ethan pamoja na Diego. Ipo siku Teresa na mpwa wake walikuwa wakiongea kuwa, kipindi cha nyuma walikuwa na mtoto wa kuasili lakini hawajui sasa atakuwa wapi. (kunakitu kimeanza pia kujitokeza).

Ni kawaida ya Ethan kumpokea madam Teresa wakati wakiwa chuoni, lakini safari hii wanafunzi walianza kumtania Ethan kuwa anamtongoza. Ethan kwa hasira alianza kupigana nao. Lakini pia Diego aliingilia ugomvi kwa hasira na kumtandika mtu kupita kiasi hadi Ethan akajiuliza kwanini ameonekana kuwa na hasira na wale wanafuzni kupita kiasi?

Dondoo zijazo: Siri nzito yapangwa kufichuliwa, ni kuhusu wazazi halisi wa Margaux, je siri hii itamgusa kiasi gani Ceyn ambaye amekwisha jitawala katika jumba la kifahari?

Fuatilia dondoo zijazo hapa hapa Asili Yetu Tanzania na karibu tena!

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.