Header Ads

Breaking News
recent

AsiliYetuTz: TAMTHILIA YA "HER MOTHER'S DAUGHTER" YAFIKA PATAMU.


Baada ya marafiki wa nne kusambaratika kimahusiano huku wakikabiliana na hali ngumu ya maisha, sasa waanza kurudisha mahusiano yao kwa njia tofauti tofauti.

Liam baada ya kugundua kuwa yeye na mdogo wake ni watoto waliozaliwa nje ya ndoa, sasa wafukuzwa na mke halisi wa Antonio ambaye ni baba yao. Liam kwa hasira anamchukuwa mdogo wake pamoja na mama yake mzazi na kuamua kusafiri hadi kwa bibi yao ambaye ni mama wa mama yao.

Wakiwa huko Liam aliamua kuhamishia masomo yake, ambapo pia baada ya rafiki yake Margaux kuamua kuondoka nyumbani kwao kwa sababu ya kutompenda Celyn naye aliamua kuhamishia masomo yake huko japo haikuwa rahisi kufanya hivyo, kwani siku alipofika huko aliibiwa vitu vyote na kubaki njia panda.

Baada ya Margaux kuondoka nyumbani sasa Celyn aonekana kutawala ndani ambapo wazazi wake wapya wanajaribu kumridhisha kila wakati, na kumsahaulisha alikotoka.

Ethan bado maisha yake na mama yake hayaendi vizuri, kwani yeye bado anachakalika na kazi za kutengeneza magari, kwani hata chuo hakufanikiwa kuhitimu kwani baada ya mama yake kuumwa ilimbidi atafute pesa kwa udi na uvumba. Hadi sasa Ethan ameamua kumhamishia mama yake kwa shangazi yake ili akapate matibabu kule.

Baada ya visanga vyote kufanywa na Margaux, sasa aamua kurejea nyumbani na kukubari kufanya kazi katika kampuni yao ya "Memorata". Lakini pia Celyn amepewa zawadi ya ofisi mpya katika kampuni hiyo ya "Memorata" ingawa amemuomba baba yake asimchukulie kama mtu maalum sana bali awe kama mfanyakazi wa kawaida.

Je kurudi kwa Margaux ni kwasababu ya kuendelea kupambana na Celyn? au anaanzisha mchezo mwingine mchafu? Baada ya Liam kufika kwa bibi yake, bibi yake alimuomba afanye kazi katika duka lake la kuuza samani za ndani. Alikubali na kuianza kazi hiyo kwa ufanisi mzuri uliowavutia wengi.

Ghafla Ethan akiwa anatembea anamuona Margaux akiwa ndani na kuamua kumfuata. Pale Ethan alimuuliza Margaux "umeamua kurudi tena?" lakini pia  Margaux alimuuliza "vipi nawewe ulihitimu chuo?" Ethan kwa majonzi alimjibu "hapana sikuweza kuendelea na chuo kwasababu mama yangu alikuwa akiumwa hivyo nilitafuta kikazi kidogo ili nipate kipato cha kumtibia mama yangu". Ethan alimuaga Margaux na kuondoka, lakini Margaux alionyesha uso flani wa huzuni na kutaka kama kumuita, lakini alishindwa.

Kwa upande wa babu yao Celyn na Margaux anawataka kila mmoja awe mfanyakazi wa kampuni yake, lakini kila mmoja wapo aliyeulizwa alikataa na kutaka kufanya kazi katika kampuni ya baba yake. Je mzee ataamua nini?

Baba yake Liam anaumwa hivyo Liam na familia yake wameamua kurudi kwao kwa muda mfupi baada ya baba yao Antonio kuwaita, lakini pia kumbuka kwa sasa mahusiano ya Liam na Celyn yamekatika kwani Celyn hataki tena. Baba yake Liam anamuita Julio baba yao akina Celyn na Margaux na kumwambia, "share yangu iliyoko katika kampuni yako, nataka mwanangu Liam aitumie, hivyo aingie katika kampuni".

Je nini kitatokea pindi Liam atakapokutana na Celyn na Margaux katika ofisi moja? Fuatilia dondoo za Tamthilia hii ya "Her Mother's Daughter" hapa hapa Asili Yetu Tanzania Blog. Karibuni Sana!.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.