Header Ads

Breaking News
recent

TAMTHILIA YA "HER MOTHERS DAUGHTER" SEHEMU YA 30 - MAPENZI YAZIDI KUWACHANGANYA.

Celyn na  Margaux
Ilipofikia Tamthilia hii ni tamu ni baada ya Ethan kuachana na mpenzi wake Margaux, sasa balaa lazidi kumuandama Ethan kwa baba yake kutiwa lumande, huku mama yake mzazi akilazwa kutokana na mshituko alioupata baada ya kuambiwa kuwa mume wake kakamatwa.

Margaux hataki tena kusikia wala kumuona Ethan tena, hivyo anajaribu kuishi maisha bila ya mpenzi wake wa hapo nyuma. Margaux ameendelea na msimamo wake wa kuto msamehe Celyn bali ameendelea kumtuhumu kuwa na mahusiano na Ethan.

Ethan naye kutokana na mzongo wa mawazo, inambidi aanze mahusiano ya karibu sana na Celyn ili kuipooza nafsi yake. Hatahivyo kwa upande wa Margaux naye tayari Liam naye amekwisha tupa ndoano na kumnasa Margaux. Lakini cha kushangaza tayari Margaux anaingiwa na wivu kuwaona Liam na Celyn muda mwingi, hivyo anamwambia Liam huku machozi yakiwa yanambubujiaka kuwa, chagua unaye mtaka, mimi au huyo Celyn, lakini Margaux anamsisitiza Liam kuwa amchague yeye, kwasababu ndiye aliyebaki akimtegemea ampe upendo wa kweli.

Baada ya baba yake Ethan kukamatwa, Ethan alimfuata Margaux usiku chumbani kwake, akipitia njia za panya na kufanikiwa kumuomba amuombee msamaha kwa babu yake ili amuachie baba yake. Lakini Margaux alikataa kata kata huku akimwaga machozi.

Tayari Margaux amegundua kitu kati ya mama yake Celyn na Julio baba yake. Margaux alimfuata Teretha na kumuambia kuwa amekwisha fahamu kuwa yeye anauhusiano na baba yake, pia akahidi kuwa atamwambia mama yake yani Beatrice.

Margaux sasa amekwisha mwambia Celyn kuwa mama yake ndio chanzo cha matatizo yote, lakini Celyn alipomuuliza mama yake, alikataa kata kata. Baada ya bibi yake Margaux kugundua njama za mume wake, sasa mpatia Celyn Scholarship ya kwenda kusoma nje.

Huku Margaux naye apewa Scholarship na babu yake, lakini Margaux adai familia yao nzima wahamie kule anakoenda. Lakini kwaupande wa baba yake ameonekana kukataa kwenda, huku mke wake akilazimisha waondoke wote.. Mpaka sasa Julio hajamwambia mkewe Beatrice kuwa, Celyn ni binti yao.

Je nini kitaendelea ambapo Beatrice atakapogundua kuwa Celyne ni binti yao? Je nini kitatokea Ethan atakapogundua kuwa Liam ni mpenzi wa Margaux? Fuatilia dondoo hizi hapa hapa.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.