HER MOTHERS DAUGHTER SEHEMU YA 33 & 34, SASA MAMBO YOTE NJE NJE.
![]() |
| Liam na Celyn |
Teresa akiwa katika shughuli zake za kuuza viatu gengeni, mara mafisa wa polisi wanajitokeza na kumkamata na wengine kwa kosa la kuuza gengeni. Habari zinamfikia Julio kupitia kwa Celyn. Julio anakuja kumtoa Teresa polisi, lakini wakiwa nje mara Beatrice anatokea na kuwafanyia fujo huku akimtuhumu mume wake kuwa na mahusiano na Teresa.
Julio aliamua kuvunja ukimya na kutoboa siri kuwa Celyn ni binti yao walio mpandikizia Teresa mbegu za Julio na Beatrice, lakini baada ya hapo akatoweka kwa miaka mingi bila wao kujua kilichokuwa kikiendelea.
Baada ya Celyn kumkuta mama yake akilia, na kuambiwa ni Beatrice ndiye aliyemfanyia fujo, basi alienda hadi kwa akina Beatrice na kufanya fujo za kutosha. Lakini wakiwa bado katika timbwili hilo, Teresa, baba yake na mama yake walifika hapo. Beatrice alikuwa mkali kwa Teresa, lakini mama yake kwa ghadhabu alimwambia "usimkalipie dada yake kiasi hicho". Neno hilo liliwashangaza sana Margaux na Celyn, kwani hawakuwahi kujua kuwa mama zao ni ndugu.
Kilichofuata ni siri kutobolewa kuwa Celyn ni binti yao. Margaux kusikia hivyo aliondoka kwa ghadhabu na kumpigia simu Liam ili amfuate, lakini pia baada ya Celyn kujua kuwa ni binti yake Julio, naye alitoka nje na kwenda kukaa bara barani. Wakati Liam akimfuta Margaux alimkuta Celyn akiwa amekaa pembeni ya bara bara akilia. Celyn alimuomba Liam amchukuwe aende naye mbali kabisa, duh! Liam kwa upande wake ilikuwa furaha. Kwani alimchukuwa hadi ufukweni.
Na baada ya hapo waliamua kuchukuwa chumba hotelini na kulala mzungu wa nne, kwani Celyn alikuwa akihofia sana kufanya chochote kwani hakuwahi kufanya upuuzi wowote kabla. Lakini wakiwa mapokezi, kunawadada wawili waliwaona na kuwachukuwa picha.
Kwa upande wa Ethan amefanikiwa kupata nyumba na kumhamishia kule mama yake. Mambo bado mabichi kabisa, kwani Beatrice bado haamini kuwa Celyn ni binti yao, adai wafanye vipimo vya vina saba (DNA). Picha za Celyn na Liam za vuja na kumfikia Margaux, vipi kuhusu Ethan ataamua nini?
Karibu tena Asili Yetu Tanzania kwa dondoo zijazo.

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA