Header Ads

Breaking News
recent

PICHA YA BEYONCE ILIYODAIWA KUMKUFURU YESU KRISTO.

Mtandao wa hip hop morning umeelezea jinsi msanii wa muziki wa majuu maarufu kama "Beyonce" alivyoonekana kuwakela watu wengi nchini Marekani hasa wale wakristo.

Mwanadada Beyonce, inasemekana juzi kati tarehe 30 ya Desemba 2013 alitupia picha hiyo hapo juu inayomuonesha Beyonce akiwa amekaa mbele ya meza kubwa, ambapo nyuma yake kuna picha ya wanafunzi wa Yesu wakiwa wameketi pamoja  naye.

Lakini Beyonce ameonekana kuziba nafasi ya Yesu Kristo katika picha hiyo, kitu ambacho kimezua utata mkubwa mno kuwa, huenda Beyonce amejifananisha na Yesu au anajaribu kujifanya yeye ndio yesu au amepindua utawala wa Bwana Yesu Kristo.

Kitendo hicho kimewakera wakristo wengi duniani, kwa msanii huyo kutoheshimu Imani za Wakristo. Hatahivyo wengine wameibuka na mtazamo mwingine kuwa, huenda mwanamuziki huyo akawa naonyesha nembo za mpinga Kristo.

Tujiulize mimi na wewe!!!

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.