Header Ads

Breaking News
recent

VIJANA TUCHANGAMKIE FURSA ZINAPOJITOKEZA, TUSIWAACHIE WENYE MITAJI TU.

Ajira kwa vijana bado ni shida hapa nchini, lakini pia mengi  yanajitokeza katika kupunguza makali ya ajira hapa nchini, lakini pia itabaki kuwa ndoto kwa wale tunaosubiri ajira itufuate hadi pale tulipo. Kunafursa baadhi za ujasilia mali zinajitokeza kila kukicha, japokuwa nyingi hazikupi pesa bali zinakupa maarifa ama elimu ya kupata pesa, kuzizalisha, kupanua biashara, kuhimiri ushindani katika soko n.k.

Usidharau fursa yoyote inapotokea katika eneo lako, kwani kunamafunzo mengi yanajitokeza katika maeneo yetu lakini vijana kwa asilimia kubwa hudharau na kuwaachia wenye elimu ndio washiriki fursa hizo. Lakini ukweli ni kwamba fursa zilizo nyingi za kijasiliamali huwa hazibagui elimu.

Kwa kiwango kikubwa wanawake huchangamkia fursa zinazojitokeza hata kuliko wanaume na ndio maana wanapiga hatua katika biashara zao. Vijana tujitokeze kwa wingi tunapopewa fursa. Kufunguka kiakili, ni zaidi ya kupewa mtaji halafu usijue jinsi ya kuutumia. Tuwe wabunifu hata kama hatuna mtaji wa kuanza kujiajiri, tuanze kujiajiri kiakili na kisha kifedha. Karibuni Asili Yetu Tanzania.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.