TAMTHILIA YA WALANG HANGGAN (My Eternal) - NATHAN BAADA YA KUPIGWA VIBAYA NA DANIEL, AJICHOMA KISU TUMBONI.
![]() |
| Kushoto ni Margret akiwa na Johana |
Familia ya Marco Montenegro inazidi kuvurugwa na jina la Katherina, kwani Nathan anaonekana kutokuwa sawa bila ya kuwa na Katherina. Johana naye anajikuta ndani ya vugu vugu hilo baada ya kushirikishwa katika utekaji wa Katherina.
Miss Henya naye baada ya kupewa ujumbe wa Nathan kutaka kuwauwa Daniel na Katherina, sasa naye anamfuata Daniel kijijini na wote kujikuta wakiingia matatizoni.
Huko kijijini baada ya Katherina kumueleza ukweli Daniel kuwa Nathan alimbaka, sasa Daniel anaondoka huko kwa hasira hadi nyumbani kwao Nathan na kuwakuta wote hapo nyumbani. Mbele ya baba yao Daniel anatoboa siri kuwa Nathan na Johana ndio waliohusika kumteka Katherina. Daniel pia anamuonya Nathan mbele ya baba yake kuwa aachekumfuatilia Katherina.
Marco Montenegro anashangazwa na kusikia kuwa wanae ndio waliomteka Katherina. Anaamua kufanya uchunguzi ili kubaini ukweli, lakini akiwa bado hajabaini lolote, Nathan anachukua kisu huku akijaribu kuzuiwa na Johana lakini Nathan anamfuta Daniel.
Magari yote yanafunga break, Daniel anashuka na kukutana na Nathan mara ugomvi mzito unazuka. Baada ya Nathan kuzidiwa anachomoa kisu na kuanza kukitumia, lakini Daniel anafanikiwa kumdhibiti na kumpa kichapo cha nusu kuuwa. Wakati ugomvi huo ukiendelea Johana alikuwa akiangalia, Daniel anachukua kisu kile na kutaka kumchoma kwa hasira, lakini anaahirisha na kumuacha Nathan chini akiwa amelowa damu.
Wakati Johana akifanya juhudi za kutafuta msaada, mara Daniel anamuita kwa nyuma na kuchukua kile kisu na kumuambia Johana kuwa "utanipeleka hospitali", akajichoma kisu tumboni.
Baada ya Nathan kuwahishwa hospitari na kupewa matibabu, Nathan nawaambia polisi kuwa alichomwa kisu na Daniel, lakini Johana anaaonekana kutomsaidia kwa asilimia kubwa kaka yake, kwani alipoulizwa na polisi alidai kuwa kile kisu kilikuwa cha Nathani.
Nathan anamlazimisha Johana amsingizie Daniel ili kulipiza kisasi, lakini Johana anaonekana kutokubaliana na hilo. Tayari Daniel ameanza kusakwa na polisi huko aliko kwani kuna mtu ameripoti kumuona Daniel. Je Johana atamsariti Daniel? Je Nathan atachukuwa hatua gani?
Daniel anaonekana kumpa kichapo Miguel - mtu hatari, lakini pia askari anaonekana kumteka Daniel, je atamkamata? Katherina nae kama anaujauzito hivi, je niwanani kama ni kweli? Karibu kwa dondoo zijazo hapa hapa Asili Yetu Tanzania.
+at+Johanna(Melissa)+para+pigilan+ang+kasal_1.jpg)
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA