Header Ads

Breaking News
recent

KATIKA TAMTHILIA YA MY ETERNAL (Walang Hanggan) NDOA YA NATHAN YAWA BATILI HUKU KATHERINA ANASA MIMBO YA NATHAN.

Daniel na Katherina wakicheza Tamthilia ya Walang Hanggani
  Utamu wa Tamthilia ya "Walang Hanggan My Eternal" sasa wazidi kipimo baada ya mastaa wote waliocheza tamthilia hiyo kuanza kufichua siri za uovu walioufanya kipindi chote cha mchezo huo.
 

Tokea mashabiki waanze kutazama uhondo wa Tamthilia hii hawakuwahi kufahamu kuwa mama yao akina Thomas na Katherina kuwa yuko hai bado. Ukutupilia mbali hilo lakini pia katika juhudi zote za Nathan kutaka kumrudisha Katherina kwake akiwa kama mke wake, zimekuwa ni batili.

Hata hivyo Emily naye tayari anagundua kuwa ofisini kwake kumetegwa kamera kila sehemu na hata kampuni ya Thomas imegundulika kuwa sii ya Thomas bali ni ya Miguel.

Katherina anasindikizwa na Daniel kutoka huko mafichoni kuja mahakamani, lakini wakati mahakama inaendelea, Daniel anaamua kujificha na na kumfuata mama yake kazini kwake ili wasalimiane kwasababu ni siku kadhaa tokea walipoacha kuonana. Daniel anafanikiwa kuonana na mama yake, lakini wakati anaondoka katika jengo hilo, ghafla anamuona miguel na kumuita kwa sauti kubwa kwani Miguel alikuwa anataka kupanda gari.

Miguel alisimama kumtazama Daniel, lakini Daniel alionekana ni mtu mwenye hasira sana, ghafla akamrukia Miguel na kuanza kugombana nae. Daniel alifanikiwa kumdhibiti Miguel na kumfunga kamba na pembeni aliandika ujumbe uliosema "huyu ni muuwaji". Daniel alifanya hivyo ili polisi wakifika wamkamate Miguel, lakini kabla ya yote Thomas alifika na kumkuta boss wake Miguel amefungwa kama.

Thomas anamfungua na kujifanya alifungua mwenyewe na kumpiga Thomas, hivyo polisi walivyokuja hawakumkuta Miguel. Kule mafichoni walikopewa hifadhi Katherina, Ihenya na Daniel, kumbe mama huyo aliyewapa hifadhi ndiye mama yake kina Thomas na Katherina. Hii imegundulika baada ya Daniel kumbamba huyo mama akiwa ameshikilia picha ya familia nzima ya Katherina yeye, Thomas, Katherina na baba yao. Daniel anaamua kutoboa siri kwa Katherina.

Sakata la kesi ya Nathan na Katerina limeelekea kusambaratika baada ya Nathan kuambiwa na bibi yake Margret kuwa, siku ya ndoa yao walipofungishwa na mchungaji haikuwa sahihi kwani kibali chake cha kufungisha ndoa kilikuwa kimekwisha muda na hivyo sekretari wake alizembea kwenda kukilipia kiongezwe muda (renew) hivyo mchungaji baada ya kugundua alimuita Margret na kumueleza, lakini Margret kwasababu hakutaka Nathan amuoe Katherina basi alitumia nafasi hiyo kuficha ukweli.

Baada ya Nathan kujua ukweli kuwa ndoa yake ni batili anachukia sana na kumtimua wakili wake na kusema "siwezi kuwekeza tena katika ndoa batili". Sasa anaunda tena kikundi cha majambazi ili kumsaka Daniel na Katherina.

Kathrina bado ni mja mzito japokuwa anaugua mara kwa mara. Kathrina sasa baada ya kumfahamu mama yake anaonekana kumkasilikia mama yake kwasababu aliwaterekeza miaka mingi iliyopita, lakini mama huyo kwa kukubari makosa anamuelezea Kathrina mkasa mzima na kuomba msamaha.

Thomas naye anamjua mama yake mzazi je atachukua hatua gani? Atamkubali au atamkana? Kamera zimefichuka katika ofisi ya Emily na Emily amegoma kuacha kazi, tayari kunajambo anataka kulifanya, je ni jambo gani hilo? Nathan na majambazi wake wanafanikiwa kumpata Katherina huku wakimteka Miss Ihenya, je Daniel jinsi alivyo hatari kwa mapigano ataruhusu njama za Nathan ziendelee? Karibu Asili Yetu Tanzania kwa dondoo zaidi.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.