Header Ads

Breaking News
recent

BONGE LA TAMTHILIA WALANG HANGGAN - DANIEL AKUTANA NA MIGUEL USO KWA USO LUMANDE.

Daniel na Katarina
Daniel alikuwa kama dhahabu vile kwani kila hasimu wake alikuwa akimtafuta kwa hali na mali, japokuwa kila walipokutana uso kwa uso basi cha moto walikiona. Nathani na majambazi wake wanajipanga kwa ghadhabu na kutumia muda mwingi wa kumsaka Daniel na Katarina.

Nathan anafanikiwa kufika alikojificha Katarina na kutaka kumteka, lakini wakiwa katika purukushani ghafla Daniel anafika na kumkabidhi Nathan kipigo na kutoroka na Katarina. Wakati Katarina wakitoroka, Daniel alitoboa tairi ya gari la Nathan.

Nathan anamteka bibi yake Daniel Miss Ihenya na kumpigia simu Daniel ajisalimishe yeye na Katarina, lakini kabla ya hapo Emily ameripoti polisi kuwa ametegewa kamera ofisini kwake, hivyo Miguel amekamatwa na kuwekwa lumande.

Baada ya Katarina kumjua mama yake ambaye anaitwa Luisa sasa anarudisha moyo wake nyuma na kumkubali na kumsamehe, lakini kwa Thomas inakuwa vigumu kwani amekataa kumsamehe kwa sasa kwasababu aliwaacha na baba yao tokea wakiwa wadogo.

Nathan na kikundi chake wanamvizia Daniel na kumpiga na kwasababu alikuwa akitafutwa na polisi kwa kosa la kumpiga polisi na lile la kusingiziwa na Nathan kuwa amemchoma kisu, sasa akamatwa na kuwekwa ndani. Emily na Marco wanafanya juhudi za kumdhamini Daniel lakini bado, huenda akasubili hukumu ya hakimu.

Johana dada yake Nathan ndiye anayejua ukweli wote wa mkasa wa Nathan na Daniel, sasa aanza kutokubaliana na kitendo cha kumsingizia Daniel. Je mahakamani ataeleza ukweli? Au atamtetea kaka yake Nathan? Daniel awekwa chumba kimoja na Miguel lumande, je maadui hawa wawili wataishi chumba kimoja? Miguel baada ya kumuona Daniel lumande, anampigia simu Thomas ampelekee sigala na pesa nyingi, huenda ni za kuwahonga wafungwa wampige Daniel...... Fuatilia dondoo zijazo hapa Asili Yetu Tanzania.




No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.