Header Ads

Breaking News
recent

TAMTHILIA YA WALANG HANGGAN EPISODE YA 49 - PENZI LA NATHAN NA KATHERINA LAINGIA DOA.

Nathan
 Baada ya mikiki mikiki ya bomu kuripuka huku Miguel akitokomeoa pasipojurikana na kitita cha fedha za kampuni ya Emily Gidoti, sasa kampuni hiyo huenda ikafirisika kutokana na deni kubwa aliloliacha Miguel.

Emily na mwanae wanaanza kupanga mbinu za kumtafuta Miguel ili arudishe fedha ili kunusuru kampuni dhidi ya deni kubwa la milioni miatatu linalolikabili kampuni ya Gidoti. Magreth naye anazidi kusutwa, sasa ni dada yake Ihenya ambaye baada ya kupokea kichapo kutoka kwa Miguel na kukimbizwa hospitali sasa amepona na kurejea nyumbani.

Kwa mara ya kwanza Marko na mwanae Daniel wanatamka hadharani kutaka kurudiana na wapenzi wao wa zamani. Kwa upande wa Marko amefunga safari hadi nyumbani kwa Emily na kutamka wazi wazi kuwa bado anampenda Emily na anataka arudiane nae ingawa huko nyuma kunaupinzani mkali kutoka kwa familia yake yani wanae Nathan na Johane pamoja na mama yake mzazi Margret.

Tayari Miguel amekwisha anza kutumia fedha alizotaperi kampuni ya Emily Gidoti, anunua jumba la kifahari nje ya mji pasipojulikana na kuwaita wafanyakazi wake yani Thomas na mwenzie na kuwakabidhi donge nono kila mmoja.

Hapo nyuma Daniel Gidoti alimripia deni Thomas na kumuajili kuwa mfanyakazi wake mpaka pale atakapozilipa fedha hizo, lakini cha kushangaza ghafla Thomas anamlipa Daniel fedha zote alizokuwa anadaiwa na kumwambia, hivi karibuni mtafirisika na utakuwa mfanyakazi wangu tena.

Kwa upande wa Daniel Gidoti anamtamkia Nathan kuwa atampora mke wake Katherina ambaye alikuwa ni mpenzi wa Daniel zamani. Tayari Daniel amemrudishia Katherina shamba kubwa la alilokuwa amelinunua kutoka kwa kaka yake Katherina yani Thomas, ikiwa ni ndoto zao wote wawili kuja kuishi katika eneo hilo.

Kaka yake Katherina yani Thomas amefichua siri nzito alizomfundisha Nathan ili akubaliwe na Katherina. Siri hizo alizisikia kutoka kwa Daniel akipanga mikakati ya kumridhisha mpenzi wake Katherina. Badaada ya Katherina kupewa siri ya mumewe Nathan, sasa baada ya kurejea nyumbani anamuwakia Nathan na kutamka jambo ambalo Nathan alibaki mdomo wazi...... je ni maamuzi gani hayo? Fuatilia hapa.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.