TAMTHILIA YA "MY ETERNAL" WALANG HANGGAN- DANIEL ANUSULIKA KUFA KWA BOMU.
![]() |
| Daniel Gidoti |
Baada ya Miguel kusuka njama za kumtupilia jela Daniel sasa kibao kimemgeukia yeye mwenyewe baada ya Daniel kugundua jumba kubwa lililokuwa likitumika katika kuhifadhi vifaa vya kulipulia mabomu na ambavyo vilitumika kumlipua mke wa Marko.
Miguel alidanganya paspot zake lakini kila aliyetaka kumchunguza aliingia katika dimbwi zito la hatarini. Ihanya yule bibi anaeishi kwa Emily alijaribu kuingia chumbani kwa Miguel na kufanikiwa kuziona paspot za Miguel zilizokuwa zikionyesha tarehe ya tukio la ulipuaji wa ndege alikuwa huko huko. Lakini bibi huyo akiwa bado chumbani humo, Miguel alimbamba na mwisho wake alimtandika chuma kichwani na kukimbizwa hospitali.
Lakini akiwa hospitari Miguel alimtuma Thomas akamuuwe ili asije kutoa siri, lakini juhudi hizo ziligonga mwamba mara kwa mara alipojaribu. Mguel anampenda sana Emily lakini Emily hamuamini sana Miguel hivyo hataki kuingia katika penzi hilo.
Miguel baada ya kuona hapendwi na Gidoti sasa anapanga njama ya kumfirisi Emily Gidoti, anaitisha mkutano na wenye hisa katika kampuni ya Gidoti na kutaka uzarishaji wote wa kampuni hiyo uhamie nje ya nchi hivyo aliwasiliana na Magreth ambaye pia anahisa katika benki moja hivi na kuomba mkopo wa dola milioni mia tatu kwa jina la kampuni ya Gidoti.
Lakini siku moja Emily anashikwa na machale na kuingia ndani kwa Miguelna kufanikiwa kuzichukua zile paspot na kumpelekea Daniel ambaye alikuwa akifanya upelelezi kwa kujificha kuhusu Miguel.
Daniel anafanikiwa kwenda hadi getini kwa kina Nathan, akiwa maeneo yale mara Katherina anatokea na kuanza kugonga geti lakini mlinzi hakumsikia, ile anageuka nyuma akamuona Daniel wakakumbatiana na kuanza kukumbushia mapenzi yao. Lakini ndani kwa bahati mbaya Nathan anawacheki katika security camera na kusoma mpango mzima.
Nathan akatoka nje na bastola na kuanza kumlenga Daniel, alimkosa risasi nyingi lakini baba yake ndiye aliye msaidia. Huku kwa Emily ni kasheshe kwani amegundua njama iliyotumika kumfirisi tena na muhusika akiwa ni Magreth na Miguel.
Marko baada ya kugundua kuwa mama yake ameshiriki utapeli huo anaamua kumtimua kwake. Daniela nae baada ya kunusurika kufa kwa bomu, anaamua kuhama kwao Nathan na kumuahidi kumpora Katherina na kumrudisha katika himaya ya penzi lake la zamani. Nathan anachukia sana.........
Fuattilia dondoo za Thamthilia hii hapa hapa Asili Yetu Tz.

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA