PICHA: HILI NDILO GALI LENYE MITAMBO YA UPELEZI LILILOKABIDHIWA KWA JESHI LA POLISI.
Jeshi la polisi nchini limepokea msaada wa gari maalum lenye mitambo
itayoweza kufanya upelelezi,ukaguzi na uchunguzi wa kitaalam
utakaosaidia kupata ushahidi wa uhakika katika kupambana na matukio ya
uharifu hapa nchini.
Akiziungumza na waandishi wa habari, baada ya kusaini hati za
ushirikianao wa jeshi la polisi la Uturuki na kisha kukabidhiwa gari
hilo, mkuu wa jeshi la polisi nchni,insepcta jenerali Saidi Mwema
amesema baadhi ya waharifu wamekuwa wakihachiwa huru na mahakama kwa
sababu ya ushahidi wa jeshi la polisi kutokamilika kutokana kutokuwepo
na vifaa vya kitaalam ambapo amesisitiza vifaa vilivyomo katika gari
hilo vitasaidia kukusanya taarifa za uhakika za matukio ya uharifu.
Kwa habari zaidi bofya hapa ITV TANZANIA

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA