Header Ads

Breaking News
recent

TAMTHILIA YA WALANG HANGGAN "EPISODE 3&4" - WIVU WA MAPENZI WATANDA KATI YA KATERINA NA DANIEL.

Kateria - jina lake katika mchezo mpya
Daniel na Katerina wanakuwa wote pamoja katika nyumba moja, lakini wote wawili wanajikuta wakiwa na hisia za kimapenzi huku kila mmoja akimuonea wivu mwenzake mara anapokutana rafiki mpya.

Daniel ni mtoto wa mtaani aliyeokotwa na dada yake Margret na kuamua kuishi nae. Siku moja baba yake Katerina akiwa katika mizunguko yake, alivamiwa na watoto wa mtaani na kufanyiziwa, lakini Daniel akiwa mdogo alijitokeza na kuwafukuza watoto wale na kumsaidia baba huyo.

Baba yake Katerina aliamua kumchukuwa hadi kwa bibi yake na kuamua kuwapa kazi ya usaidizi nyumbani kwake. Daniela alionekana kuanza kupendana na Katerina wakati wakiwa wadogo, kwani Daniel alionekana kumsaidia Katerina wakati kaka yake alipokuwa akimuonea.

Siku moja wakati Daniel na Katerina  wakiwa wakubwa japo Katerina alikuwa hajafikisha miaka 18, wote wakiwa shambani, Daniel aliokota pete nzuri ya uchumba, pete ambayo Katerina alionekana kuipenda na kuitaka kwa hali na mali.

Daniel aliikatalia na kusema atampatia msichana atakaye mchagua, Katerina alijisikia wivu sana kwani alikuwa akimpenda sana Daniel na kumwambia kila wakati kuwa yeye ndiye mshichana wake na sio mwingine.

Vituko vya Katerina vinaanza kama alivyokuwa akifanya katika tamthilia iliyopita ya "Mara Clara" ambapo aliigiza kama CLARA. Katerina akiwa shule wakati akiondoka kwenda nyumbani ghafla anatokea kijana mmoja na kumkomalia ampatie namba yake huku akijaribu kumshawishi ili siku iliyofuata ahudhulie katika sherehe yake huko Manila.

Katerina anampatia namba yake ya simu, lakini yule kijana wakati akitaka kuondoka, akambusu shavuni na kuondoka. Kumbe tayari Daniel alikuwa akitazama mchezo wote wakati akiwa amemfata Katerina ili ampeleke nyumbani. Daniel anaamua kumfuatilia yule kijana na kumkunja kisawa sawa, na kumuonya.

Katerina bado hajaridhika kumfanyia vituko Daniel, kwani ameshamuonyeshea matukio kama hayo kwa wavulana wawili, ambapo lengo kuu ni kumnasa kikamilifu Daniel na kumuweka katika himaya yake ya kimahaba. Kwani Katerina amekwisha onyesha dalili za wazi za kutaka kukiss na Daniela, lakini bado anazinguliwa.

Sasa Katerina anatimiza miaka 18, siku aliyokuwa akiisubiri kwa hamu, kwasababu Daniel alimkatalia kufanya nae kitu chochote hadi akiwa mtu mzima. Siku ndio imefika, wameandaa sherehe kubwa sana. Umefika wakati wa Katerina kuwasiri katika ukumbi.... Daniel hakuamini macho yake, kwani aliona mtu kama maraika akishuka na nguo kubwaaaaa kama ya bibi harusi yeah!! alikuwa ni Katerina!!!!

Emily mchumba wa  zamani wa Marco Montenegro, ambaye alifungwa jela na kujifungua mtoto aliyesemekana kufariki, sasa ameonekana kutoka jela na kunawili sana, na ile pete aliyonayo Daniel ni ya Emily.

Je, Daniel ameonekana kuiandaa kumvisha Katerini, atamvisha kweli? Na je, Emily kama alivyomuahidi Mama yake Marco kuwa atamnyang'anya kila kitu alichonacho ili kulipiza kisasi, ndivyo itakavyokuwa?

Je nini kitaendelea?  Karibu tena kwa dondoo  nyingine za tamthilia hii hapa hapa.

1 comment:

  1. pamoja asili yetu nafatilia matukio mbal mbal mpo juu

    ReplyDelete

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.