EPISODE YA 54 - "TAMTHILIA YA MARA CLARA" – GARY ADHAMINIWA HUKU AMANTE NAE ATOKA HOSPITALI, WOTE WAKUTANA.
![]() |
| MARA |
Amante apata fahamu na kuongea na Alvira, wote waombana
msamaha na kurudiana, lakini kwa upande wa Gary hali bado ni tete, kwani
anampigia simu Clara ili amdhamini kutoka polisi.
Clara afanikiwa kumtoa baba yake polisi, lakini anajaribu
kumshinikiza wahamie nyumba nyingine kwani hiyo ni mbaya, lakini Gary
hajakubaliana na wazo hilo kabisaaa!.
Gary anampigia simu Alvira na kumtaka wakutane kwa maongezi
lakini, Alvira anakataa na kusema yeye ndio chanzo cha mambo yote yaliyotokea,
akaongeza kwa kusema “nenda kuzimu”.
Clara aenda hospitali kuomba wazuie kesi ya baba yake Gary
isipelekwe mahakamani, lakini maombi hayo yanatupiliwa mbali na familia ya
Amante, aondoka hospitali kwa hasira.
MARA na SUZAN wanaenda
kumuona mama yake Gary mwenye ugonjwa wa kupooza, wanamuuliza kama Clara anajua
au anashiriki katika maovu ya Gary? Pia bibi huyo anaomba waondoke naye, wanafanikiwa
kutoroka nae na kutokomea kusikojulikana.
Gary anarudi na kumuuliza mlezi wa mama yake (Mrs. David)
kwa ukali huku akimkaba shingoni, “mama yangu yukowapi?” Anaamua kumfukuza ili akamtafute mama yake
hadi ampate kwani asipompata atamuua. Gary na Clara wanaamua kwenda kuripot
polisi, lakini polisi wanamwambia hawawezi kumtafuta mtu yeyote anayedhaniwa
kupotea hadi masaa 24 yapite. Gary anakasilika na kuanza kujibizana na polisi,
lakini Clara anamwepusha na kuondoka kituoni hapo.
MARA na Suzan wafanikiwa kumtorosha mama yake Gary na kwenda
nae katika nyumba mpya ya Alvira, huko nyumbani bibi huyo anaanza kupata nafuu
ya kuweza kuongea. Amante anatoka hospitali na kujumuika na familia yake upya,
lakini Amante anaanza kumuuliza mama yake Gary kuhusu maovu ya mwanae ili apate
ushahidi wa kumtupa jela.
Gary, Clara wote wanakutana na familia ya Amante uso kwa
uso, sasa nini kitatokea kati yao?
Je nini kitaendelea? Tazama Star TV na karibu tena kwa dondoo nyingine za tamthilia hii hapa hapa.

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA