TAMTHILIA YA “MARA CLARA” EPISODE YA 53 – GARY AWEKWA RUMANDE, HUKU AMANTE AKIRUDIWA NA FAHAMU ZA KUWEZA KUONGEA.
![]() |
| GARY |
![]() |
| ALVIRA |
Suzan na MARA na Derick wanafanikiwa kurejea jijini, lakini
wanapokea Ujumbe mbaya wa Amante kupigwa risasi. MARA na Suzan wanafika nyumbani. Mama yake
Gary anawaonyesha kitu kwa kusonta huku akiwa amejawa na uchu wa kusema kitu, lakini wakati
aking’ang’ana kuwaonyesha, Clara anaingia na kuanza kujibizana na vibaya na
MARA. MARA namwambia Clara “sikujua kuwa wewe na baba yako Gary mnahusika na
kutaka kumuuwa baba yangu, sasa basi wewe na huyo baba yako mtakwenda wote jere”.
Vilio vya tanda hospitali baada ya Alvira kufika hospitali
kumuona mumewe Amante, kiukweli anajuta na kutubu kwa makosa yote aliyomtendea
mumewe. Lakini wakati akizungumza maneno hayo, tayari Gary alikuwa kajibanza
sehemu akitazama picha yote, kitu kinachomfanya aghadhabike maradufu na kuanza
kupiga ngumi ukuta. Jamaa anaamua kurejea nyumbani akiwa ni mwenye hasira,
anamkuta Clara na kumweleza kuhusu Alvira, lakini kibaya zaidi Clara anamwambia
kuwa “nilikwambia mapema kuwa mama
hakupendi” maneno hayo yalimuongezea Gary hasira na kujikuta akimkaba
shingo Clara.
Alvira anampigia simu Suzan na kudai kuongea na MARA,
alishindwa kuongea bali alimwambia kuwa hali ya baba yake ni mbaya huku
akimwaga machozi kama mvua. Gary pia nampigia simu Alvira na kumueleza kuwa
yuko nyumbani anakula good time, japokuwa alimtaka arejee nyumbani.
![]() |
| AMANTE |
Gary anamkuta Clara akiwa anaelekezwa nje na bibi yake kwa
kumnyooshea kidole nje. Gary anang’amua eneo zilipofichwa pesa na kuzifukua pesa
hizo zilizokuwa zimechimbiwa na bibi huyo. Tayari Clara amekwisha fanya shoping
na kurejea nyumbani, lakini bibi yake anamuomba Clara awasaidie MARA na Suzan,
lakini Clara anakataa.
Alvira anarejea nyumbani na kumkuta Gary, Alvira anaulizwa
kuwa alikuwa wapi? Lakini Gary anajibu mwenyewe “unatoka kwa Amante!” Alvira kwa jazba anamjibu kuwa “ninae mpenda ni Amante sio wewe”,
anakimbia kujifungia ndani huku akiomba msaada kwani Gary tayari alikuwa
kashikilia bastora. Gary anabomoa mlango na kumkamata mkono kwanguvu Alvira. Alvira kwa hasira anazidi kumuambia
hampendi na anamchukia kwani anampenda Amante.
Alvira akiwa anapiga kelele za kuomba msaada, MARA na Suzan
walikuwa wamefika nyumbani kwa Alvira na kusikia kelele, wote wanawafuata huko
chumbani. Gary kuona hivyo, anatoa bastora na kumnyoshea Suzan lakini Alvira na
MARA wanamzingira Suzan kwa pamoja, lakini Gary bado akiwa na hasira anawauliza
“mnafikiri mtakimbia kwenda wapi?” anawanyooshea bastora wote watatu. Wakiwa
bado wanajibizana maaskali wanafika, na Avira anawaamuru wamkamate, anakamatwa
na kuwekwa ndani.
Huko hospitalini Amante anapata nafuu na kumuulizia Alvira.
Clara afanikiwa kufika hospitali kumuona Amante,Je Clara analipi la kufanya
ilihali baba yake Gary yuko rumande? Je Gary ataendelea kukaa rumande?
Je nini kitaendelea? Tazama Star TV na karibu tena kwa dondoo nyingine za tamthilia hii hapa hapa.



No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA