TAMTHILIA YA “MARA CLARA” EPISODE YA 51 NA 52 – “GARY” AMPIGA RISASI “AMANTE” NA KUWANYOOSHEA BASTORA ALVIRA, SUZAN NA “MARA” KWA PAMOJA.
Njama ya Gary David kutaka kuzindua mapenzi ya zamani kati
yake na Alvira, sasa yatinga katika sura
ya mbele zaidi, kwani Alvira amkana mumewe Amante mbele ya Gary na kusema hamtaki
tena na anataka kuwa na “Gary David”.
Amante kwa kiasi
kikubwa anajihisi kama sanamu kwani hakuamini macho na masikio kwa kile
alichokisikia kutoka kwa Alvira kuwa hamtaki tena na anamtaka Gary! Amante kwa sasa anaishi kwa yule bibi
aliyekuwa akiwafanyia kazi ambaye Alvira aliamua kumtimua kwa kile alichodai
kuwa anaingilia mambo yake binafsi huku akiwa kama kibaraka wa Amante. Bibi
huyo anajaribu kurudi kwa Alvira na kumsihi aachane na Gary lakini juhudi hizo zinagonga
mwamba.
Alvira anaendelea na uchunguzi wa mauwaji ya Lenita pamoja
na mabomu aliyonusulika mwanae MARA. Alvira anafunga safari hadi kwa mama yake
Lenita na kumpeleleza kuhusu Lenita, lakini pia juhudi hizo zinagonga mwamba
pale mama huyo anapokosa kumuona jambazi aliyekuwa na mwanae Lenita kwani
alifanikiwa kumuona siku za nyuma.
Alvira bado anajaribu kumpeleleza mama yake Gary na kumsihi
kuwa “najua Mrs. David unampenda mwanao Gary, lakini nikishakamilisha ushahidi
nitamrudisha tena mwanao jela”, bibi yuko tayari kutoa siri ya mwanae lakini
bado hajaweza kupata muda wa kutosha, huenda akipona kitanuka kwa Gary.
Amante apigwa risasi shingoni, na mtu ambaye huenda akawa
Gary, lakini pia mamayake mara aonekana kuwa na dalili za mwanzo za kuwa na
ujauzito ambao amehisi ni sikuile ya mwisho ambayo mume wake Gary alimlazimisha
wakalala nae ambapo asubuhi yake alitoroka na MARA na kutokomea pasipojulikana.
EPISODE YA 52 GARY AANZA KUMUONYESHA ALVIRA UNYAMA - INAENDELEA
HAPA
Baada ya Amante kukosa ushahidi wa kutosha kwa Gary, sasa
aamua kumfuatilia katika bishara yake mpya haramu ya dawa za kulevya ili apate
sababu ya kumtupa jela Gary. Huku nyumbani kwa Alvira mahusiano yake na Gary yanathibitika
baada ya Alvira kutamka mbele ya Amante na Gary kuwa hampendi Amante na bali
anampenda Gary peke yake.
Gary anatoa maoni kwa Alvira “nikwanini tusimuondoe Amante duniani
ili aache kutuingilia penzi letu?” Alvira anashtuka na kukataa kata kata na
kumwambia Gary asijaribu kuingilia na kumdhuru Amante kwani huo ni ugomvi wao,
na pia Amante bado ni mumewe wa ndoa. Alvira anaanza kuutambua moyo wa Gary kwa
matendo anayoanza kumuonyesha.
Gary anaanza kama kumlazimisha Alvira wanyonyane ndimi, pia ahamie kwa Alvira,
lakini Alvira kwasababu malengo yake sio kuolewa na Gary ni kutafuta vidhibiti
vya maovu ya Gary, hivyo anamwambia Gary asiwe na haraka ya mambo, muda utafika
tu.
Huko kijijini Suzan anapata vipimo kuwa ni mjamzito,
ujauzito unaosemekana kuwa ni wamumewe Gary. MARA adhamilia kabisaa kurudi
nyumbani kwao, lakini Alvira anamsihi Suzan amzuie kwani huko mambo bado sii mazuri. Huku mjini Clara nae amerejea
tena huku akiendeleza kumfanyia bibi yake ugaidi.
Mama yake Gary anapata nafuu ya kuweza kutembea japo kwa
shida, hadi alikochimbia zile fedha za Gary. Akiwa bado anachimbua, mfanyakazi
wake anaanza kumtafuta huku akisaidiana na CG,wanamkuta japo alikuwa bado
hajazitoa.
Amante anajipanga yeye na wenzake ili kumfuatilia Gary
katika biashara zake za dawa za kulevya, anafanikiwa kuchukua video kwa njia ya
simu, lakini wenzake Gary wanashtukia kuwa kunamtu anawafuatilia, hivyo
wanamwambia Gary. Amante akiwa bado ananyata kuondoka mara Gary anatokeza kwa
nyuma yake na bastora na kusema “Amante leo sitokuacha, huwezi kuondoka”, Gary
anampiga risasi na Amante kuanguka chini.
Nyumbani kwa Gary
yeye na Clara wanafanikiwa kuzifukua zile pesa zilizokuwa zimefukiwa na mama
yake. Amante afanikiwa kufikishwa hospitali, huku Suzan na MARA wafanikiwa
kurudi na kufika hospitali kumuona Amante.
Gary anafika hospitali na kumkuta Suzan na MARA, anatoa
bastora na kumnyoshea Suzan lakini Alvira na MARA wanamzingira Suzan kwa
pamoja, mara Gary bado akiwa na hasira anawauliza “mnafikiri mtakimbia kwenda
wapi?” anawaonyooshea bastora wote watatu. Huku Madaktari wanajaribu kumpiga
shoti Amante ili azinduke lakini juhudi kama zinagonga mwamba hivi!, Je nini
kitaendelea?
Je nini kitaendelea? Tazama Star TV na karibu tena kwa dondoo nyingine za tamthilia hii hapa hapa.

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA