EPISODE YA 50 TAMTHILIA YA “MARA CLARA” – “AMANTE” ATOKA JELA NA KUMFUMA MKEWE “ALVIRA” AKIWA NA “GARY” – ‘ALVILA’ AMFUKUZA “AMANTE”
Familia ya Amante Deville inazidi kusambaratishwa na Gary ikiwa
ni baada ya Alvira kumuajiri Gary kuwa kama dereva wake, lakini kumbe kila
mmoja ananjama nzito na mwenzake.
Gary anazidi kuongeza ukaribu mkubwa nyumbani kwa Amante ili
hali akijua kuwa Amante yuko jela hivyo anatumia nafasi hiyo, kujenga mazoea ya
karibu sana na Alvira (mke wa Amante). Lakini Yule bibi ambaye ni msaidizi wa
kazi wa nyumbani kwa Amante anaonekana kuwa na wasi wasi na Gary kuajiriwa
katika nyumba hiyo.
Bibi anamfuata Alvira na kumtahadharisha kukaa mbali na
Gary, lakini Alvira analichukulia swala hilo kitofauti kabisa na kuona kuwa
anaingiliwa katika maaamuzi yake binafsi. Siku hiyo hiyo bibi huyo anatoka nje
na kumkuta Gary akiwa nafuta gari vumbi na kumuuliza kulikoni yuko pale? Gary
anamuelezea kuwa ameajiriwa pale kama dereva, lakini Yule bibi kwakuwa
anafahamu ugomvi wa Gary na Amante siku nyingi basi alimuonesha Gary hali ya
kutoridhishwa na uwepo wake pale.
Gary anagundua kuwa bibi huyo ndiye anayemshawishi Alvira
amfukuze kazi. Gary anajipanga huku usoni akiwa amevaa kininja na kumnyatia bibi huyo wa kina Amante usiku wakati akitoka
kutupa uchafu, anamkaba shingo na kumkandamiza, lakini huko ndani Alvira
anahisi kerere nje na kulazimika kuja kumtafuta bibi huyo nje, hapo ndipo
alipoachiwa shingo na Gary kutokomea.
MARA huko aliko anaumia mkono baada ya kwenda kuachanisha
ugomvi wa Derick (mototo wa boss wao) kijana aliyemuokoa wakati amedumbukia
majini. Licha ya MARA kuanza kuzoea mazingira ya huko aliko, kama ameanza
kuzoeana na Derick kiaina hivi.
Clara bado yuko kati kati kwani vitendo vya baba yake Gary
kuvamia vamia kwa Amante kama vinaanza kumkera hivi, kwasababu siku aliyomkaba Yule
bibi, baada ya dakika chache kukabwa, Garl alifika pale nyumbani kwa Amante
haraka. Lakini swali moja Yule bibi alimuuliza, ni umejuaje tukio hili
limetokea ukaja haraka? Gary alijitetea kuwa, nilipigiwa simu na Clara
akihitaji msaada wangu, kiukweli Clara hakupendezwa na hilo lakini kishingo
upande ilibidi akubali.
Yule bibi alifunga safari hadi jela na kukwenda kumuambia
kilichotokea kwake na akimuomba amzuie mkewe Alvira asimruhusu Gari kuendelea
kufanyakazi pale. Siku ya pili Avira anafika jela kumtembelea Amante, lakini
amante anaonekana kutokuwa na furaha. Amante anamkalipia na kumuambia amfukuze
Gary nyumbani kwake na kusema au wanauhusiano wa kimapenzi na Gary? Alvira
anakasilika na kumpiga kofi, mwisho kila mmoja wanaachana wakiwa wamenuniana.
Lakini mwanasheria wa Amante anafanikiwa kunasa video ikimuonyesha Gary
alivyoenda kumuuwa Christina na hiyo ilisababisha Amante aachiliwe na kurejea
nyumbani.
Alvira anamtembelea mama yake Gary aliyepooza nyumbani,
akijua kwamba kunakitu bibi huyo hutaka kumuambia kila siku lakini inashindikana.
Siku ya kwanza bibi huyo anamuonyesha pesa zilipofukiwa lakini akiwa bado
anashangaa mara Gary anawakuta. Siku ya pili bibi anafanikiwa kumuandikia
kwenye karatasi neno ”pesa”. Lakini Alvira katika kuificha katika mkoba wake
anaidondosha pale chini na kuiacha pale pale. Gary anaikuta na kushtukia mchezo
hivyo anamrazimisha mama yake aseme pesa zilipo, lakini pia Alvira amekwisha
anza kung’amua kuwa huenda ni zile pesa walizotozwa kwa MARA na CLARA.
Amante anatoka jera na kumkuta Gery akiwa na Alvira nyumbani
kwake, aliamini kuwa watu hao walikuwa na mahusiano ya kimapenzi, hivyo
alimgombeza mkewe Alvira kwa kitendo hicho.Hiyo haikutosha tuu alimtandika
ngumi ya shavu Gary mpaka chini. Alvira anakasilika na kumfukuza Amante. Huko
mama yake MARA ashikwa na wasi wasi kuwa
huenda akawa mja mzito, je ujauzito wanani? Je Amante wataachana na mkewe
Alvira?.
Je nini kitaendelea? Tazama Star TV na karibu tena kwa
dondoo nyingine za tamthilia hii hapa
hapa.

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA