LULU (ELIZABETH MICHAEL) APATIWA DHAMANA KUINGIA URAIANI.
![]() |
| Elizabeth Michael ‘Lulu’ akisubiri dhamana mahakamani. |
MSANII maarufu wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael
‘Lulu’ amepata dhamana leo baada ya kukidhi masharti aliyowekewa na mahakama.
Dhamana hiyo imetolewa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu, jijini Dar es Salaam baada ya hoja za mawakili wanaomtetea kukubalika.
Masharti aliyokuwa amepewa ni pamoja na wadhamini wawili
wafanyakazi wa serikali wenye kiasi cha Sh. milioni 20 kila mmoja na
kuwasilisha pasi ya kusafiri ya msanii ili kutotoka nje ya nchi hadi kesi hiyo
itakapokamilika.
Huku mashabiki wake na baadhi ya wasnii wenzake wakiwa na
furaha mahakamani hapo, kila mmoja alisikika akisema Mungu mkubwa.
Source: Global Publishers

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA