AMAZON 'AJITOA' MTANASHATI ENTERTAINMENTS
![]() |
| Amazon |
Staa wa singo ya 'Mamito' ambayo iko juu hivi sasa kwenye
vituo kadhaa vya redio hapa Bongo, Justin Kobelo 'Amazon' ametangaza rasmi
kujiondoa kwenye kundi la Mtanashati Entainments linaloongozwa na Ostaz Juma na
Musoma kwa kile alichokiita ubabaisha katika masuala ya uongozi na mikataba ya
kazi.
Akizungumza Exclusive na Teentz.com mapema leo,Amazon
amefunguka kuwa tangu kujunga na kundi hilo hakuwahi kupatiwa fursa ya kurekodi
nyimbo yoyote mpya achilia mbali
Checherumba ambayo amearifu kuwa aliirekodi kabla ya kujiunga na kundi
hilo.
"Yaa! ni kweli kuwa nimeamua kuondoka Mtanashati
kuepuka ubabaishaji mkubwa uliopo ndani ya kundi hilo ambalo mkurugenzi wake
amekuwa akiwanyima nafasi wasanii wengine na kuwapendelea baadhi akilenga zaidi
kujinufaisha kupitia majina ya wasanii hao" alisema Amazon
Akiendelea zaidi nyota huyo wa singo ya checherumba alisema
kuwa amechoshwa na 'uditeta' wa mkurugenzi unaofanywa na mkurugenzi wa kundi
hilo ikiwemo hatua ya kuwataka wasanii walio ndani ya kundi hilo kutia saini
mkataba wa Milele utakaowafanya kuwajibika ndani ya kampuni hiyo maisha yao
yote.
"Awali nilitakiwa kusaini mkataba wa 'milele'
ambao unakutaka kufanya kazi maisha yako
yote ndani ya kundi kitu ambacho binafsi nilikitaa kwa kuwa sijawahi kuona
mkataba wa aina hiyo sehemu yoyote ile
ingawa ajabu ni kuwa kuna baadhi ya wasanii wenzangu wameukubari"
alisema Amazon.
Stori na Dismas Ten 0718489260. (TEENTZ.COM)

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA