UPELELEZI WA ANAYEDAIWA KUMFANYIA MTOTO VITENDO VYA UKATILI MBEYA WAKAMILIKA.
![]() |
UPELELEZI wa kesi ya mwanamke anayetuhumiwa kumnyanyasa
mtoto wa dada yake kwa kumfungia ndani na kumchoma kwa maji ya moto na
kumlazimisha kula kinyesi chake, mjini Mbeya umekamilika.
Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Achiles Mulisa ameiambia
Mahakama ya Mbeya kuwa upelelezi wa kesi ya mtuhumiwa Wilvina Mkandala ,24,
umekamilika na akaomba tarehe ya kuanza kusikilizwa kesi hiyo ambapo inadaiwa alisababisha majeraha akiwa
na nia ovu ambayo imemsababishia ulemavu mtoto Aneth (3) ambaye amekatwa mkono.
Alisema upande wa Jamhuri una mashahidi wanne ambao wataanza
kutoa ushahidi wao mahakamani hapo Novemba 22, mwaka huu kutokana na upelelezi
kukamilika na akawataja kuwa ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Majengo Shukuru
Mwakanyamale, dokta Paul anayemtibu mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya,
polisi aliyepeleleza kesi hiyo, WP Pudensia na Habiba Mwakanyamale ambao wako
tayari kufika mahakamani na kutoa ushahidi wao.
![]() |
| Anayetuhumiwa Wilvina Mkandala. |
Mulisa akisoma mashtaka mbele ya
hakimu mkazi mwandamizi wa mahakama hiyo, Gilbert Ndeuruo amesema kosa
alilolifanya ni kinyume cha kanuni ya adhabu kifungu cha 222(a) sura ya 16 kama
ilivyorejewa mwaka 2002.
Mshtakiwa amekana shitaka hilo ambapo ametupwa rumande hadi Novemba 22,
mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.
Source: Global Publishers


No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA