PICHA ZA DIAMOND AKIPAKA PODA NA WANJA ZA VUJA.
![]() |
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akipaka wanja.
|
PICHA zilizosambaa mtandaoni zikimuonesha mwanamuziki Nasibu
Abdul ‘Diamond Platnumz’ akipaka wanja na ‘mapouda’ zimewashanganza wengi huku
baadhi wakisema anakoelekea siko.
![]() |
Diamond Platnumz akipaka poda.
|
Wakizungumza na Ijumaa, baadhi ya watu waliyoziona picha
hizo walisema kuwa, ni kweli kuna suala la kujiweka ‘sopsop’ kwa staa ili
aonekane nadhifu lakini hilo la kufikia kupaka
wanja na ‘mapouda’ kama mademu halileti picha
nzuri.
“Unajua watu wanaweza kufikiria tofauti kwa picha hizi,
mwanaume na poda au wanja wapi na wapi?
Ni sawa, yeye ni rais wa masharobaro lakini sidhani kama
usharobaro ni lazima upake wanja, mimi hizi picha zimenishtua sana,” alisema
Halima wa Kinondoni jijini Dar.Naye Juma Salum wa Mwenge jijini Dar alisema
ukiona watu wanafikia hatua ya kuitwa wanaume kama mabinti ni kwa matukio kama
haya kwani imezoeleka wanaojiremba hivyo ni wanawake na si wanaume.
Katika kufuatilia zaidi, mwandishi wetu alibaini kuwa picha
hizo Diamond alizipiga alipokuwa akishuti video ya wimbo alioshirikishwa na
mwanadada Keisha. Diamond alipotafutwa ili kuzungumzia ishu hiyo, hakuweza
kupatikana mara moja.
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA